SPORTS AM 02/02/2019: Boniphace Pawasa afichua kilichomfanya aonekane mnazi wa Yanga akiwa Simba

Описание к видео SPORTS AM 02/02/2019: Boniphace Pawasa afichua kilichomfanya aonekane mnazi wa Yanga akiwa Simba

Huyu ni beki wa zamani wa Kimataifa wa Tanzania Boniphace Pawasa ambaye aling’ara na klabu ya Simba SC kwa miaka minane (8) kwa mafanikio makubwa ikiwemo kuitoa Zamalek kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akiwa anaitumikia Simba, baadhi ya viongozi wake walikuwa wakimshuku kuwa yeye ni kibaraka wa Yanga na kuwa ana mapenzi na mahasimu wao hao. Pawasa ameliweka wazi hili na kusimulia kila kitu.

Hii ni sehemu ya pili ya mazungumzo yetu na beki huyu tukianza naye Jumamosi iliyopita (Januari 27, 2019) , ambaye ameendelea kusimulia historia yake jinsi alivyojiunga na Simba hadi kwenda kucheza soka la kulipwa Rwanda, DRC na Uarabuni.

Sehemu ya pili ya kipindi hiki ni habari za michezo asubuhi ya leo na sehemu ya tatu ni uchambuzi kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Al Ahly na Simba.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке