Je, Ni Ipi Familia Halisi Ya Mwanawe Saitoti?

Описание к видео Je, Ni Ipi Familia Halisi Ya Mwanawe Saitoti?

Familia ya aliyekuwa Waziri wa Usalama wa ndani marehemu Profesa George saitoti sasa imejitokeza kupinga madai ya familia moja kutoka eneo la Subukia inayodai kwamba mwanao aliyepotea miaka 24 ni Zachary Musengi, mwanawe Saitoti. Kupitia kwa wakili wa familia ya Saitoti Fred Ngatia, familia hiyo imewasilisha stakabadhi za usafiri na hata shule alizosomea Zachary, wakidai kwamba mtoto aliyepotea ni mwingine bali si Zachary. Familia ya Sebastian Maina hata hivyo inasimama kidete ikisisitiza kuwa Zachary ni mwanao, wakitaka uchunguzi wa chembechembe za urithi kufanywa ili kuthibitisha madai yao.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке