"Nilifuatiliwa Na Magari Mawili Mpaka Nyumbani | Walinishambulia Na SMG"

Описание к видео "Nilifuatiliwa Na Magari Mawili Mpaka Nyumbani | Walinishambulia Na SMG"

"Septemba 7, nimeondoka nyumbani nilikuwa Dodoma, kuna eneo linaitwa area D, kuna maghorofa mengi ndio wanakaa viongozi wa Serikali na yanalindwa muda wote nimeishi pale toka 2010. Nilifika Bungeni tukajadili na nilikuwa mtu wa mwisho kuzungumza katika ile session ya asubuhi.Nikatoka nje, nikampigia dereva wangu simu aje anichukue twende nyumbani tukale chakula cha mchana. Mimi siku zote nakula nyumbani.

Ukiwa bungeni miaka ile njia rahisi ilikuwa inapita katikati ya uwanja wa ndege sasa ilikuwa njia imefungwa sababu palikuwa panafanyiwa matengenezo Kwahiyo ili uende area D inabidi uende mjini hivyo tukaelekea mjini. Tumepita round about ya Singida, tukapita round about ya barabara ya Arusha ambayo inapakana na uwanja wa ndege tulivyopita dereva akaniambia kuna magari mawili yanatufata nyuma kwenye akili yangu nikamuulizaDereva hawa polisi wanatufuatia nini? Maana mimi huwa nasumbuliwa na polisi.

Tukafika area C tuko nao gari mbili land cruiser nyeupe na Mitsubishi tukaenda mpaka area D tumekaribia getini kama kuna mtu anafahamu iliko Club84 tulipopita pale Land cruiser nyeupe ikapaki pembeni Mitsubishi ikaja tukaingia nayo getini. Lile geti huwa linafungwa muda wote na huwa kuna walinzi wawili au watatu wanasilaha muda wote siku hii geti liko wazi na hakuna mlinzi tukapita tukaenda block E ninapoishi. Tukaingia parking bahati nzuri siku hiyo magari yalikuwa mengi na nafasi za parking zimechukuliwa imebaki moja kwa sababu niko mbele nikaingia kwenye hiyo parking.

Wakaingia upande wa kushoto wanatafuta eneo la kupaki kuna magari, kulia kuna magari wakageuza gari kuelekea walipotokea dereva akaniambia nisishuke, wakasubiri na wao. Mmoja akatoka siti ya nyuma akaamia mbele upande wa abiria wakazungumza akarudi ndani akafunga mlango ghafla akafungua yeye, akafungua mwingine wanamashine hapo wakaachia" - Tundu Lissu

#LiveOnClouds360

Комментарии

Информация по комментариям в разработке