Lissu Aachiwa Huru, Kesi Yake Kuunguruma Agosti 24

Описание к видео Lissu Aachiwa Huru, Kesi Yake Kuunguruma Agosti 24

SUBSCRIBE NOW    / uwazi1  
Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumpa dhamana mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu upande wa mashtaka umedai upelelezi umekamilika na atasomewa maelezo ya awali Agosti 24.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amempa dhamana Lissu leo, Julai 27 akisema upande wa mashtaka umeshindwa kutaja kesi ambayo mshtakiwa huyo wa kesi ya uchochezi aliwahi kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa.

Amesema hoja ya upande wa mashtaka kuwa Lissu anyimwe dhamana kwa ajili ya usalama wake haijajitosheleza kumweka ndani.

Hakimu Mashauri amesema kundi la mawakili 18 wamejitokeza kumwakilisha Lissu, hatua inayoonyesha watu wana upendo dhidi yake.

Kutokana na hayo, Hakimu Mashauri ametoa dhamana akimtaka Lissu kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao watasaini bondi ya Sh10 milioni kila mmoja.

Pia, amemtaka asitoke nje ya Jiji la Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha Mahakama.

Saa 3:50 asubuhi, baada ya kukamilisha masharti ya dhamana Lissu aliingia kwenye gari lake na kuondoka eneo la Mahakama ya Kisutu.

Lissu leo amewakilishwa na wakili Peter Kibatala kwa niaba ya mawakili wengine.
Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya…
   / uwazi1  
   / uwazi1  
   / uwazi1  
WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/
FACEBOOK:   / globalpublis.  .
TWITTER:   / globalhabari  
INSTAGRAM:   / globalpubli.  .

Комментарии

Информация по комментариям в разработке