Dakika 47 za moto hoja ya Mdee bungeni, mnyukano mkali watokea

Описание к видео Dakika 47 za moto hoja ya Mdee bungeni, mnyukano mkali watokea

Hoja ya Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee aliyetaka Bunge lijadili utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara kwa EPC+F imechangamsha mjadala wakati Bunge likiwa limeketi kama kamati kujadili mafungu ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Mjadala huo umejiri leo Mei 30, 2024 jioni huku Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson akimbananisha Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba afafanue utekelezaji wa EPC+F huku Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina akichuana vikali na Waziri wa Uchukkuzi ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa wakishukiana kwenye mjadala huo.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке