AMINI USIAMINI HILI NDIO ENEO LA BEI JUU ZAIDI KULALA TANZANIA, MILIONI 22 SIKU MOJA, UNAOGA NA PAPA

Описание к видео AMINI USIAMINI HILI NDIO ENEO LA BEI JUU ZAIDI KULALA TANZANIA, MILIONI 22 SIKU MOJA, UNAOGA NA PAPA

Inawezekana usiamini kwamba kuna sehemu zinagharimu zaidi ya shilingi Milioni 22 za Kitanzania kulala kwa usiku mmoja tu! Amini au usiamini sehemu hizo zipo, tena hapa hapa nchini kwetu Tanzania.

Thanda, ni sehemu kwa ajili ya mapumziko iliyotengenezwa na mtu binafsi katika eneo la kisiwa cha Shungimbili kilichomo Wilaya ya Kisiwa cha Mafia. Kisiwa hiki kina ukubwa wa takribani hekari 20 ambamo ndani yake imejengwa nyumba moja. Nyumba hiyo ina vyumba vya kulala vitano na vibanda viwili pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya Hindi kusini mwa Tanzania ambapo familia ya watu mpaka 10 inaweza kuishi.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке