JUMLA YA VIKUNDI 69 VIMEPEWA MIKOPO HALMASHAURI YA MPANDA, KATAVI

Описание к видео JUMLA YA VIKUNDI 69 VIMEPEWA MIKOPO HALMASHAURI YA MPANDA, KATAVI

Wanufaika wa vikundi vya mikopo kutoka halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kufanyia kazi iliyokusudiwa katika fedha za mikopo ambazo zimetolewa katika makundi ma 3, wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni utekelezaji wa Serikali katika utoaji wa mikopo Robo ya pili, 2024 / 2025.

Hayo yamesemwa na Deodatus Kangu kaimu mkurugenzi Halmashauri ya manispaa ya Mpanda wakati akizungumza na vikundi hivyo katika ukumbi wa Manispaa Mkoani Katavi.

Amevitaka vikundi vitakavyo nufaika na mikopo hiyo kufanyia kazi iliyokusudiwa fedha watakazo zipata na pia kuwa waaminifu kuzirejesha kwa wakati ili na wengine wapate mikopo hiyo.

Mgeni rasmi Sebastian Simon Kapufi ambae ni mbunge wa jimbo la Mpanda mjini amesema kuwa pesa zilizotolewa kama mkopo kwa wajasiliamari wadogo wadogo zimetolewa takribani milioni 633.4 kwa kwaajili ya kuchochea maendeo kwa makundi maalumu.

#mpandaradiofm97.0
#sauti ya katavi

Комментарии

Информация по комментариям в разработке