LISSU AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU 'WATU WASIOJULIKANA' KUPANGA NJAMA YA KUMDHURU

Описание к видео LISSU AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU 'WATU WASIOJULIKANA' KUPANGA NJAMA YA KUMDHURU

Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema kuwa amepata taarifa za jaribio la kuumizwa halafu wahusika wa tukio hilo wamsingizie Mwenyekiti w chama hicho Freeman Mbowe kwa kuwa wanamnyukano wa kisiasa ndani ya chama hicho.


"Juzi nimetafutwa sana na mmoja wa wazee wa nchi hii mmoja wa viongozi wa nchii sio kiongozi wa kisiasa hakunipata kwa sababu ya hizi hekaka. Jana nimeona misscall zake zaidi ya kumi nikamtafuta nikafanikiwa kumpata akaniambia mdogo wangu nimekutafuta sana nimetafutwa na mtu mkubwa sana kutoka serikalini huyu mtu amenifuata huku nilipo huyu mtu inabidi afatwe kwa ndege ukitaka kwenda kwa gari ni safari siku mbili kwa hiyo bwanamkubwa amepanda ndege kumfuata.

Amesema amemfuata kumuomba mzee huyo aingilie kati kwa sababu kuna mipango inapangwa inaweza kuharibu amani ya nchi .

"Akamwambia hawa humu ndani wanapanga kumuumiza Lissu halafu wamsingizie Mbowe kwa sababu ya hii mivutano inayoendelea ndani watamuumiza halafu zigo la lawama watamsukumia Mbowe"

Lissu amesema kuwa ameshauri na Mzee huyo ambaye hajamtaja jina kuwa aongeze ulinzi na kuongeza umakini.

Lissu amesema kuwa aliomba ushauri kwa huyo mzee kama anaweza kuujuza umma juu ya hatari iliyopo mbeleni kwake na kuruhusiwa ndipo alipoamua kuchapisha kwenye ukurasa wake wa X na kuzungumza kwenye vyombo vya habari.

Lissu amesema kuwa hao watu wanaweza kutumia minyukano ya ndani ya Chadema kumuumiza kisha asingiziwe Mbowe

Комментарии

Информация по комментариям в разработке