PROF JANABI ATOA SOMO KWA WANAMZUMBE KUHUSU JINSI YA KUPAMBANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Описание к видео PROF JANABI ATOA SOMO KWA WANAMZUMBE KUHUSU JINSI YA KUPAMBANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Chuo kikuu Mzumbe kupitia Skuli ya Utawala wa Umma na Menejimenti (SOPAM) chini ya mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (HEET) wameendesha mhadhara wa umma kwa wanafunzi na wafanyakazi wa Kampasi Kuu Morogoro na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro na Manispaa ili kuelimisha umuhimu wa kuzuia na kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

Mratibu wa Mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi, Chuo Kikuu Mzumbe upande wa kujenga uhusiano wa kazi na Sekta Binafsi Dkt. Albogast Musabila amemshukuru Prof. Janab kwa kutenga muda na kutoa elimu muhimu kwa afya za wanamzumbe.

"Mradi wa (HEET) unauhusino na kazi zingine hasa za kijamii, tunatamani kuwepo na makubalino ili kufanya kazi na Chuo Kikuu Mzumbe. Ni lengo letu kuona wahitimu wetu wanatembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kama sehemu ya mkakati wa Chuo hii inaweza kuleta chachu ya kuboresha mitaala yetu na kuja na kozi fupifupi” alisema Dr Musabila.

Awali akifungua mhadhara huo, Amidi wa Skuli ya Menejimenti na Utawala wa Umma Dkt. Idda Lyatonga Swai, amemshukuru Prof. Janabi kwa kukubali kuja Mzumbe na kutoa mafunzo hayo “Natambua jinsi ulivyokuwa na kazi nyingi lakini umekubali kuja kutupa elimu hii adhimu tunakushukuru sana” alisema Dr. Idda.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Prof. William Mwegoha, alimesema magojwa yasiyoambukiza kwa sasa yamekuwa ndio chanzo kikubwa cha umaskini na kusisitiza kuwa watu wengi wanapambana na magonjwa yasiyoambukiza kuliko magonjwa ya kuambukiza. Amesema watu wengi hawazingatii ulaji mzuri wa chakula na kusisitiza kuwa ujio wa Prof. Janabi utasaidia wanamzumbe kujifunza jinsi ya kuzuia magonjwa yanayoweza kuepukika kwa kufuata muongozo mzuri wa chakula ili kulinda afya.”

Naye muwezeshaji wa mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa Hosptali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Yakub Janabi ameeleza kuwa watu wengi wapo kwenye hatari ya kupatwa na magonjwa yasiyoambukiza hasa kutokana na uzito mkubwa na kutozingatia lishe bora, pia magonjwa hayo kwa sasa ndio yanasababisha vifo kwa kiasi kikubwa kama magonjwa ya moyo, kansa, kisukari.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке