MAKONDA NGORONGORO ASEMA 'SITASHIRIKI KUKANDAMIZA HAKI YA MTU' ATOA AGIZO KWA RPC, NITAPIGA NYUNDO

Описание к видео MAKONDA NGORONGORO ASEMA 'SITASHIRIKI KUKANDAMIZA HAKI YA MTU' ATOA AGIZO KWA RPC, NITAPIGA NYUNDO

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesisitiza kuwa hatashiriki kukandamiza haki ya mtu mahala popote pale atakapokuwa, huku akikumbusha kuwa nafasi wanazopata viongozi ni upendeleo wa Mungu.
“Mimi mtoto wenu na mtumishi wenu lakini nina sifa nyingi mojawapo ni sifa ya kusimamia haki na ukweli, hiyo nilikula kiapo kwamba popote nitakapokuwepo kwenye nafasi yoyote sitashiriki kukandamiza haki ya mtu na sikuishia hapo nikasema nafasi hizi tunazopata ni za upendeleo wa Mungu.
“Lakini Mungu anapotupa nafasi anataka tufanye kazi kwa watu wake aliowaumba kwa mfano wake, furaha niliyonayo chama changu cha mapinduzi (Chama Cha Mapinduzi-CCM) ambacho mimi nilikitumikia kama mwenezi,” amesema Makonda.
Makonda ameyasema hayo leo Ijumaa Agosti 23, 2024 alipokuwa akizungumza na wananchi kutoka kata 11 zilizopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha katika eneo Oloirobi, Kata ya Ngorongoro ambapo ameambatana na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, William Lukuvi.

(Imeandikwa na Faraja Masinde)

Комментарии

Информация по комментариям в разработке