KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA MORNING GLORY (THE SCHOOL OF HEALING) 07/ 08/ 2024

Описание к видео KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA MORNING GLORY (THE SCHOOL OF HEALING) 07/ 08/ 2024

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH: IBADA YA MORNING GLORY (THE SCHOOL OF HEALING) 07/ 08/ 2024

UJUMBE WA LEO: HALI YA WAZAZI JUU YA WATOTO WASIOKUWAKO.

Yeremia 31 : 15
Mathayo 2 : 17 - 18
Mwanzo 44 : 20 - 22
Mwanzo 37 : 31 - 35
Mwanzo 45 : 25 - 28

Yeremia 31 : 15

15 Bwana asema hivi, Sauti imesikiwa Rama, kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake; asikubali kufarijiwa kwa watoto wake, kwa kuwa hawako,

Mathayo 2 : 17 - 18

17 Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema,

18 Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako.

Mwanzo 44 : 20 - 22

20 Tukakuambia wewe, bwana wangu, Tunaye baba, naye ni mzee, na mwana wa uzee wake ni mdogo, na nduguye amekufa; amebaki yeye peke yake wa katika tumbo la mamaye, na baba yake anampenda.

21 Ukatuambia watumwa wako, Mleteni kwangu, ili macho yangu yamwangalie.

22 Tukakuambia, bwana wangu, Kijana hawezi kumwacha babaye, maana akimwacha babaye, babaye atakufa.

Mwanzo 37 : 31 - 35

31 Wakaitwaa kanzu ya Yusufu, wakachinja mwana-mbuzi, na kuichovya kanzu katika damu.

32 Wakaenda nayo ile kanzu ndefu, wakamletea baba yao, wakasema, Tumeona hii; basi, utambue kama kanzu hii ni ya mwanao, ama siyo.

33 Akaitambua, akasema, Ndiyo kanzu ya mwanangu, mnyama mkali amemla; bila shaka Yusufu ameraruliwa.

34 Yakobo akararua mavazi yake, akajivika gunia viunoni, na kumlilia mwanawe siku nyingi.

35 Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia.

Mwanzo 45 : 25 - 28

25 Wakatoka Misri, wakafika nchi ya Kanaani kwa Yakobo, baba yao.

26 Wakampasha habari, wakisema, Yusufu angali hai; naye ndiye mtawala katika nchi yote ya Misri. Moyo wake ukazimia, kwa sababu hakuwasadiki.

27 Wakamwambia maneno yote ya Yusufu, aliyowaambia; na alipoona magari aliyoyapeleka Yusufu, ili kumchukua, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka.

28 Israeli akasema, Yatosha! Yusufu mwanangu angali hai; nitakwenda, nionane naye kabla sijafa.



Mhubiri: Mwl. George Mwakabago

Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe: [email protected]

Комментарии

Информация по комментариям в разработке