WAKAZI VITONGOJI ITULAHUMBA WAOMBA UMEME

Описание к видео WAKAZI VITONGOJI ITULAHUMBA WAOMBA UMEME

Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Nyamagana na itulahumba kati vilivyopo katika kijiji cha Itulahumba wilayani Wanging'ombe wameiomba serikali kuptia rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania kufikishiwa huduma ya umeme kufuatia wao kusalia kuwa walinzi wa nguzo ambazo zimepita katika meneo yao

Wakizungumza na kituo hiki wananchi hao wamesema licha ya uwepo wa mpango wa usambazaji wa umeme vijijini(REA) jazilizi katika kata yao bado vitongoji vyao havijafikiwa na umeme licha ya vitongoji vya vijiji vingine jirani kufikiwa na huduma hiyo.

Wananchi hao,Alex Mhagama,Edi Mfilinge,Rahel Vasapa na Wema Mfilinge wamesema kukosekana kwa umeme katika maeneo yao kunasababisha wakose huduma za msingi kiwemo viwanda na kupelekea kutokukua kwa uchumi.



Akizungumza kuhusiana na mpango huo,Diwani wa kata ya Itulahumba Thobias Mkane amekiri vitongoji hivyo kutofikiwa mpango huo na kueleza kuwa jitihada zinaendelea ili kuhakikisha vinafikiwa na umeme.



Naye mratibu wa miradi ya usambazaji wa umeme vijijini (REA) wilaya ya Wanging'ombe Justine Dickson amesema kwa awamu ya pili B vitongoji 75 ambavyo vimepitiwa na laini kubwa ya umeme vitafikiwa na huduma ya umeme jazilizi na kueleza kuwa mpango wa serikali ni kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na umeme katika awamu ya pili C.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке