RUSSIA YASHAURI RAIA WASIENDE MAREKANI, UJASUSI WATAJWA

Описание к видео RUSSIA YASHAURI RAIA WASIENDE MAREKANI, UJASUSI WATAJWA

Russia imesema kwamba uhusiano wake na Marekani ni mbaya kiasi kwamba raia wake wameshauriwa kutosafiri kwenda Marekani, Canada au baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya kwa sababu wanakabiliwa na hatari ya kuandamwa na mamlaka za Marekani.

Msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, Maria Zakharova, amesema uhusiano wa Russia na Marekani uko katika hali ya kuvunjika kabisa.

Wanadiplomasia wa Russia na Marekani wanasema uhusiano kati ya nchi hizo mbili ni mbaya kuliko ilivyokuwa wakati wa mgogoro wa makombora ya Cuba mwaka 1962.

Uhusiano umeharibika kutokana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine, na ulifikia kiwango kibaya zaidi mwezi uliopita baada ya Ukraine kuanza kutumia makombora ya masafa marefu ya Marekani ya ATACMS na STORM SHADOW yanayotengenezwa nchini Uingereza.

Makombora hayo yalitumiwa na Ukraine kutekeleza mashambulizi ndani ya Russia
na kupelekea Russia kufanyia marekebisho sheria zake za matumizi ya silaha za nyuklia.

Saa chache baada ya mashambulizi hayo ya ATACMS na Storm Shadow, Russia ilijibu mapigo kwa kutumia makombora yake mapya ya Oreshnik, makombora ambayo yaliibua kilio nchini Ukraine na kumfanya Rais Volodymyr Zelenskyy kumbilia magharibi kuomba msaada zaidi.

“Tunawashauri raia wetu kuachana na Safari binafsi za kwenda Marekani na mataifa ambayo yanashirikiana na Marekani lwa sababu wanaweza kulengwa na maofisa wa Marekani,” amesema Zakharova ambaye amesisitiza kuwa uhusiano wa mataifa hayo uko hatarini kuvunjika.
Zaidi tazama video hapo juu.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке