Njia ya Kumjua Mungu: Teolojia Toka “Juu” au Toka “Chini” || Kujifunza Biblia: Somo 13 | 24/12/2024

Описание к видео Njia ya Kumjua Mungu: Teolojia Toka “Juu” au Toka “Chini” || Kujifunza Biblia: Somo 13 | 24/12/2024

Soma Yohana 4:46-54. Ni tatizo gani lilimleta diwani kwa Yesu, na suala halisi la msingi hapa lilikuwa nini?

Mtu huyu alikuja kwa Yesu, Nuru ya ulimwengu, lakini alikuwa ameamua kuamini ikiwa tu Yesu angemponya mtoto wake, Tunaweza kusema teolojia ya mtu huyu ilikuwa “teolojia kutoka chini.” Teolojia kutoka chini inaweka kanuni na viwango kwa ajili ya Mungu na Neno Lake. Mawazo ya kibinadamu, yakiwa na dosari na yenye mipaka na ya dhahania kama yalivyo, yanakuwa mamlaka ya mwisho ya jinsi watu wanavyolitafsiri Neno la Mungu. Ni mtego wa hatari kiasi sani kuangukia ndani yake"

Teolojia “kutoka juu,” kinyume chake, inaitikia kwa imani, na imani kwa Mungu na Neno kwanza (Yn. 4:48; Yn. 6:14, 15; 2 Tim. 3:16). Biblia inapokubaliwa kwa imani, inakuwa mfasiri wake yenyewe. Mtazamo wa ulimwengu wa Maandiko, badala ya falsafa ya zama, ndio mwongozo wa kuelewa na kufasiri maandiko. Maoni ya wanadamu lazima yatiishwe na kulitii Neno la Mungu, na si vinginevyo.

Ni lazima tuamini maneno ya Maandiko ikiwa tunataka kuamini maneno ya Yesu (Yn. 5:46, 47). “ 'Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli' ” (Yn 8:31). Ikiwa tunatilia shaka Neno la Mungu, Neno lake haliwezi kukaa ndani yetu (Yn. 5:38). “Yeye anikataaye Mimi asiyeyakubali maneno Yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi Yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayoyanena na nitakayosema nini' ” (Yn. 12:48, 49).

Kusikia Neno la Mungu ni zaidi ya upokeaji tu wa habari. Inamaanisha pia Kufanya mapenzi ya Mungu. Na hili ndilo mwitikio hai kulisikia Neno. “ "Mtu akipenda kuyapenda mapenzi Yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu mwenyewe” " (Yn 7:17).

Na kusikia huku, na kutenda, Neno la Mungu ni udhihirisho wa kumpenda Yeye. “ 'Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake' ” (Yn.14:23).

Kuna uhusiano gani kati ya upendo wetu kwa Yesu na utii? Kwa nini aina yoyote ya “utii” usiotokana na upendo uko katika hatari ya kuwa ushupavu sheria?

Комментарии

Информация по комментариям в разработке