Ziara ya Waziri wa Ulinzi na JKT Alipotembelea Makao Makuu ya JKT

Описание к видео Ziara ya Waziri wa Ulinzi na JKT Alipotembelea Makao Makuu ya JKT

Waziri wa Ulinzi na JKT, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amefanya ziara ya kutembelea Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yaliyopo Wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma.

Akimkarisha Mheshimiwa Waziri mara tu baada ya kuwasili Makao Makuu ya Kamandi hiyo, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajab Mabele alimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kutenga muda wake na kuamua kuja kutembelea Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa ili aweze kujionea majukumu yanayotekelezwa na JKT.

’’Naomba nichukue nafasi hii kukukaribisha Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa, Naamini kuwa si mara yako ya kwanza kufika hapa, kwa mara ya kwanza ulifika kwa majukumu mengine. Lakini leo umefika rasmi ukiwa Waziri wa Ulinzi na JKT kuja kutumbelea’’, alisema.

Aidha, Jenerali Mabele alitumia wasaa huo kumweleza kuwa JKT ni moja ya Kamandi za JWTZ, yenye majukumu matatu yakiwemo malezi ya vijana wa wanaojiunga na JKT kwa Kujitolea na Kwa Mujibu wa Sheria, Uzalishaji Mali pamoja na Ulinzi wa Taifa.

“Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa ni moja ya Kamandi za JWTZ, na tupo kwa ajili ya kutekeleza majukumu makuu matatu ya kuwalea vijana, uzalishaji mali pamoja na ulinzi wa Taifa’’, alimalizia.

Baada ya makaribisho hayo, Mheshimiwa Waziri alipatiwa Taarifa ya Kina kuhusu Jeshi la Kujenga Taifa. Taarifa hiyo ilihusu Dira, Dhima, na Tunu za JKT; Kusitishwa na Kurejeshwa kwa Mafunzo ya JKT; Muundo wa JKT; Vikosi vya JKT; Mkao wa JKT.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке