MAGOLI YOTE: SIMBA SC 2-3 MASHUJAA FC; (ASFC - 26/12/2018)

Описание к видео MAGOLI YOTE: SIMBA SC 2-3 MASHUJAA FC; (ASFC - 26/12/2018)

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita Simba SC wametupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) kwa kukubali kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa timu ya Mashujaa FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Mchezo huo umepigwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kushuhudia Mashujaa wakitandaza kandanda la uhakika na la kujihami licha ya Simba iliyopanga kikosi cha pili kumiliki zaidi mpira na kutangulia kupata bao dakika ya 18 kupitia kwa Paul Bukaba.

Kipindi cha pili Mashujaa walitulia na kufanya mashambulizi ya kushtukiza yaliyozaa matunda dakika ya 47 wakipata bao la kusawazisha kupitia kwa Shabani Hamis na kisha kufunga la pili kupitia kwa Jeremiah Josephat.

Clatous Chama aliyeingia dakika ya 61 aliiamsha safu ya kiungo ya Simba iliyokuwa ikionekana kuelemewa na kufanikisha kupata bao la pili dakika ya 78 likifungwa na Paul Bukaba tena baada ya kipa wa Mashujaa kuutema mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Clatous Chama nje kidogo ya boksi.

Katika hali ya maajabu, Mashujaa walipata bao la tatu katika dakika ya 90+3 zikiwa zimeongezwa dakika 7 kwa shuti jepesi la chinichini lililomponyoka mlinda mlango wa Simba Deogratius Munish ‘Dida’ wakati akijaribu kulidaka.

Hadi mpira unamalizika, Simba 2, Mashujaa ambayo ni timu ya jeshi kama ilivyokuwa kwa Green Warriors (walioitoa Simba mwaka jana), wakiwa na magoli 3.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке