Mpina aliamsha jimboni amtaka DED, DC kurejesha Sh50 milioni za wananchi

Описание к видео Mpina aliamsha jimboni amtaka DED, DC kurejesha Sh50 milioni za wananchi

Baada ya mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kusimamishwa bungeni, sasa amegeukia jimboni kwake ambako amewavaa Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Fauzia Ngatumbura na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meatu, Athuman Masasi kuhusu Sh50 milioni zilizodaiwa kuchukuliwa kwa wananchi waliotozwa faini kwa kutokuwa na vyoo.

Mpina amewaka wakuu hao warejeshe fedha hizo zilizodaiwa kuchukuliwa kwa wananchi hao, huku baadhi wakidai walitozwa fedha licha ya kuwa na vyoo.

Wakizungumza jana Jumamosi Septemba 7 2024 na Mpina katika ziara yake ya kutembelea vituo vya uandikishaji wa daftari la kudumu la wapigakura, wananchi hao walidai kuwa, vyoo ambavyo havijapauliwa kwa bati pia vilitozwa faini.

Akizungumza na wananchi katika kata za Nzanza, Mwabusalu na Tindabuligi, Mpina amesema : "Naamini hizi fedha zimekusanywa kinyume cha sheria na ni uvunjifu wa sheria kuzikusanya kutoka kwa wananchi kwa makosa ya kuwasingizia na kuwaonea. Hii ni dhuluma.

“Naagiza mkurugenzi na mkuu wa Wilaya ya Meatu warudishe fedha kwa wananchi wote waliopigwa faini ndani ya siku saba kama hawatafanya hivyo, nitachukua hatua zaidi ambazo mimi nazijua."

Hata hivyo, Mwananchi imezungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meatu, Athuman Masasi aliyefafanua kuwa operesheni hiyo ilifanyika kwa lengo la kutekeleza sheria ya usafi na mazingira na kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu.

“Hatujafanya kwa lengo la kumkomesha mtu yeyote, operesheni hii ilikuwa ya amani na hakuna mwananchi aliyepigwa au kutishiwa,” amesema Masasi.

Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке