UKO WAPI (OFFICIAL VIDEO) - Christ the King Cathedral Choir - Bungoma

Описание к видео UKO WAPI (OFFICIAL VIDEO) - Christ the King Cathedral Choir - Bungoma

Performers: Christ the King Cathedral Choir - Bungoma
Producer: Verony Productions Ltd.
Copyright ©Verony Productions Ltd.

MTUNZI: J. Shomaly

Uko wapi, ndugu yangu uko wapi?
Uko wapi kanisani na wajiita ni mkristo. * 2

Foleni ya kutoa sadaka, wewe hauko,
Kwenye meza yake Bwana Yesu wewe hauko,
Jumuiya zinapokutana, wewe hauko,
Hata kutoa fungu la kumi, wewe hauko,
Uko wapi wewe bado wajiita ni mkristo. * 2

Ushirikiano wako jiulize uko wapi,
Kanisani jumuiya washiriki namna gani,
Familia yako waitunza vipi,
Nawe uko wapi?

Wengine wanapotoa wewe unajitazama,
Wakienda kupokea wewe bado watazama,
Kishawishi kipi kinachokusonga,
Nawe uko wapi?

Jumuiya wakutana wewe waomba ruhusa,
Michango inapofika shida kwako haziishi,
Na ni siku ipi shida zitaisha,
Nawe uko wapi?

Shida zinapokukumba unamkumbuka Mungu,
Zikipungua kidogo unamsahau Mungu,
Jiulize sana, tena uamue,
Ujirekebishe.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке