Rais Ruto aagiza makundi mbalimbali kuteua wawakilishi kwenye mazungumzo ya kitaifa

Описание к видео Rais Ruto aagiza makundi mbalimbali kuteua wawakilishi kwenye mazungumzo ya kitaifa

Ofisi ya rais imeanzisha mpango wa kuhusisha vijana katika mazungumzo siku mbili baada ya Rais William Ruto kukataa kutia saini mswada wa fedha wa mwaka 2024 kuwa sheria. Barua kutoka kwa mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei imewataka washikadau kutoka sekta mbalimbali kuwasilisha majina ya wawakilishi katika kamati itakayobuniwa ya kutatua maswala yaliyoibuliwa na vijana wakati wa maandamano ya kupinga mswada huo. Na kama vile Emily Chebet anavyoarifu, Rais William Ruto aliendeleza mikutano yake na viongozi wa kidini katika ikulu ya Nairobi, leo akikutana na maaskofu kutoka kanisa la (AIPCA).

Комментарии

Информация по комментариям в разработке