CCM YAPOTEZA MWANASIASA MKONGWE MUHIMU SANA RAIS-OMO-MAKAMU-MBETO-AMANI WAKUBWA WASHIRIKI MSIBA WAKE

Описание к видео CCM YAPOTEZA MWANASIASA MKONGWE MUHIMU SANA RAIS-OMO-MAKAMU-MBETO-AMANI WAKUBWA WASHIRIKI MSIBA WAKE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk, Hussein Ali Mwinyi amewaongoza wananchi na Viongozi katika mazishi ya Mwanasiasa Mkongwe Marehemu Bi.Mvita Mussa Kibendera aliefariki jana.

Mazishi hayo yamefanyika tarehe 27 Agosti 24 katika Makaburi ya Mwanakwerekwe.

Mapema Rais Dk, Mwinyi alijumuika na Waumini wa dini ya kiislamu katika sala ya maiti katika Msikiti wa MUSHAWWAR Mwembeshauri , Wilaya ya Mjini , Mkoa wa Mjini Magharibi.

Marehemu Mvita Kibendera aliezaliwa mwaka I945 wakati wa uhai wake aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama Cha Mapinduzi na Serikali ikiwemo Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM,Katibu wa CCM wilaya ya Mjini na Mwenyekiti wa CCM jimbo la Kikwajuni.

Baada ya Mazishi Alhaj Dk, Mwinyi alifika nyumbani kwa Marehemu Maungani kuwafariji na kuwapa pole wafiwa na kuwataka kuwa na subira wakati huu wa msiba mzito.

Viongozi mbali mbali waliojumuika katika mazishi hayo ni pamoja na Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman Makamu wa Pili wa Rais.Mh.Hemed Suleiman Abdullah ,Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdallah,Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe.Zubeir Ali Maulid,Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Dk.Mwinyi Talib Haji ,Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabih na Viongozi mbalimbali.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке