HIVI NDIVYO KADA WA CHADEMA ALIVYOTEKWA NDANI YA GARI, MASHUHUDA || KONDAKTA WA BASI LA TASHRIFF

Описание к видео HIVI NDIVYO KADA WA CHADEMA ALIVYOTEKWA NDANI YA GARI, MASHUHUDA || KONDAKTA WA BASI LA TASHRIFF

Gari mbili zilizokuwa na namba za usajili zisizo za kawaida, ndizo zilizotajwa na mashuhuda kuhusika katika tukio la ukamatwaji wa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema, Ali Kibao Ijumaa ya Septemba 6, 2024.

Kwa mujibu wa mashuhuda tukio hilo lilitokea saa moja jioni, muda ambao tayari giza lilishaanza kuingia na hakukuwa na aliyekuwa na wasiwasi kwa kuwa walidhani wakamataji ni askari wa Jeshi la Polisi.

Kibao, alikamatwa Ijumaa ya Septemba 6, 2024 Tegeta mbele ya Jengo la Kibo Complex na siku moja baadaye mwili wake uliripotiwa kupatikana Ununio, jijini Dar es Salaam akiwa ameuawa huku uso wake ukiwa umeharibika kiasi cha kutotambulika.

Mwili wake ulipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na ulifanyiwa uchaguzi wa kitabibu na taarifa yake bado haijawekwa wazi. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amedai kifo cha Kibao kilikuwa cha mateso na uso wake ulimwagiwa tindikali.

Leo Jumatatu, Septemba 9, 2024, Mwananchi imefika Tegeta alikokamatwa Kibao ambako ni umbali wa takriban mita 20 kutoka Jengo la Kibo Complex, ni eneo ambalo aghalabu mabasi yanayoelekea Tanga, Moshi na Arusha husimama kupakia abiria.

Kama ulivyo utaratibu wa kawaida, basi la Tashriff alilokuwa amepanda Kibao lilisimama kupakia abiria kwa mujibu wa mashuhuda, gari mbili zenye namba nyeupe ambazo zimeandikwa kwenye vibao vyeusi.

Shuhuda huyo ambaye ameomba hifadhi ya jina lake, amesema gari moja iliegeshwa mbele ya basi hilo na lingine liliegeshwa nyuma ya basi hilo, kisha watu wanne walishuka kwenye gari hizo.

“Wanne wote walikuwa na risasi (akimaanisha bunduki) alienda kwenye mlango wa basi na wawili wakaingia ndani, wawili walibaki mlangoni,” amedai.

Alichokisikia shuhuda huyo ni kauli kutoka kwa mmoja wa watu hao kuwa, ‘tumemfuata mtu wetu’ na kwa namna walivyokuwa kila mmoja alidhani ni polisi.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке