"Ruge Akiniona Ataniajiri" Meena Asimulia Siku Ya Kwanza Kuingia Mjengoni | SALAMA NA MEENA PT 2

Описание к видео "Ruge Akiniona Ataniajiri" Meena Asimulia Siku Ya Kwanza Kuingia Mjengoni | SALAMA NA MEENA PT 2

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460

MARASHI YA KARAFUU…

Jina lake halisi ni Muhaymeena Ally na kwa kifupi aliona Meena litamfaa sana na si Amina kama watu wengi wanavyodhani. Mzaliwa halisi wa Zanzibar na ni mtoto wa Stone Town kabisa. Kutoka alikozaliwa Meena na nilipozaliwa mimi si mbali kabisa, kwao Malindi karibu kabisa na bandarini na mimi kwetu ni Kiponda, wakati Meena anazaliwa mwaka 1993 mimi nilikua darasa la sita, msichana kabisa na pengine nilishaanza kuandikiana barua na kichimvi na kina Murad 🤣.

Mimi na yeye tumefahamiana hapa Dar es Salaam lakini, sina hakika kama wazazi wetu wanajua maana bado sijamuuliza Mama yangu ila nna hakika wa asilimia 99 kwamba Kaka zangu (ambao wengi wao ni wavuvi) wanawajua wazazi wake na pengine shangazi na wajomba zake, mtaa ambao Meena kazaliwa ndo njia wanayopita kwenda Pwani so uhakika huo nnao kwa asilimia hizo. Lately mimi na yeye tumekua karibu, uzanzibari pengine unachangia kwa kiasi kidogo ila binafsi zaidi ni kwasababu na admiration ya kazi zetu kwa kila mmoja wetu. Wakati Meena anakuja EATV mimi sikumbuki vizuri na nadhani zilikua ndo siku zangu za mwisho mwisho kuwa muajiriwa pale au pengine nlikua tayari nlikua nafanya mambo yangu pembeni kwa kupitia Mkasi TV.

Nilifurahia kila sekunde ya maongezi yetu haya kwasababu nilikua naongea na Rafiki yangu na ki ukweli ilikua inatakiwa yafanyike siku nyingi tu ila kama unavyojua, sisi binadamu tunapanga mambo yetu ila Mwenyezi Mungu ndo hutupa nguvu na wasaa wa kutufanya tuyatekeleze kwahiyo wakati huu ndo ulikua wakati sahihi.
Kama mwezi umepita Meena alipata mitihani kwenye mitandao ya kijamii baada iliyokua inalazimishwa iwe video yake akiwa anafanya ngono kutambaa mitandaoni. Kama Dada ilinishtua mara ya kwanza na uzuri ni yeye mwenyewe ndo alinitumia, ukimuangalia yule Dada kwa pembeni unaweza kudhani ni yeye ingawa kama unamfahamu Meena kwa ukaribu basi utajua kabisa yule si yeye. Mtihani ulikua mkubwa, mtihani wa kuwaelezea binadamu ambao baadhi yao walikua wanataka yule awe yeye nao walikuwepo lakini walikua hawataki kuamini nao pia tulikua wengi tu. Mawe mengi yalirushwa na ilihitaji Meena awe kwenye ubora wake, kuto panic na kufanya yote yaliyokua yanatakiwa kufuatwa ki SHERIA na mengine tuiachie Mamlaka inayohusika ambao naamini bado wanaendelea na kumtafuta aliyeanzisha uvumi ule na yangu imani watampata ili awe mfano kwa wengine.
Sina hakika sana na nasema hivi kwasababu kwa mtu mwenye imani na akili timamu hawezi kufanya unyama kama huu kwa mtu mwengine ambae hana ubaya nae. Madhara yanayokuja na shutuma kama hizi ni makubwa sana, ki akili na ki utu na ki biashara. Athari zake zinaweza kuwa za muda mrefu kuliko wengi wanavyo dhania.

Humu nilimuelewa vizuri, utulivu wake kwenye kujibu maswali na jinsi alivyokua amejibeba, mmoja anaweza kuangalia kwa kujifunza kutoka kwake, Meena ana kila kitu ambacho kinaweza kikamfanya yeye aweze kutimiza ndoto zake, kuwa chochote kile ambacho atapewa au atapata nafasi ya kukifanya, kuanzia kwenye filamu mpaka yote yale ambayo anatamani kuyafanya na anaweza kuyafanya kwa asilimia 100, ambayo sina shaka atayapa na pengine zaidi.

Humu tunamzungumzia Marehemu Bibi yake ambaye kifo chake kilimuathiri kwa kiasi kikubwa na jinsi ambavyo alijikwamua kutoka kwenye wimbi hilo la msongo. Maelewano yake na wazazi wake ni kitu cha kumfanya mtu ajifunze kutoka kwake, najua si kila mmoja wetu ana mahusiano ya aina hii na wazazi wake ila kwa kuskiliza naamini utapata ujumbe flani. Heshima na kujituma kwake anapokua anafanya kazi pia itaiskia humu, kujitoa kwake na jinsi anavyoangalia na kujifunza mengi kwa kuwasoma watu na nafasi zao kunamfanya aweze kufika mbali, na yangu matumaini nnayoyaona mimi kwake basi na yeye anayaona hivyo na zaidi. Kazi yetu sisi ni ku enjoy tu kwa kuangalia safari yake ya kikazi na kushuhudia mafanikio yake tele yajayo In Shaa Allah.

Enjoy hii session kama ambavyo umekua uki enjoy na kujifunza mengi kutoka kwa wengi waliopita na wengi wajao. Mungu katubariki na watu wengi wa aina hii ambao wako mbele yetu, maisha yao ni darasa tosha kwetu sote. Ni vyema yale tutakayo yapenda tukayaweka na sisi katika maisha yetu ili tufike mbali zaidi.

Love,
Salama.

Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs

Listen our Podcast on
Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa

Soundtrack Yeah by @MarcoChali    • Marco Chali Feat One The Incredible &...  

Follow:
Twitter:   / yahstonetown  
Instagram:   / yahstonetown  
Facebook:   / yahstonetown  

Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

Комментарии

Информация по комментариям в разработке