Logo video2dn
  • Сохранить видео с ютуба
  • Категории
    • Музыка
    • Кино и Анимация
    • Автомобили
    • Животные
    • Спорт
    • Путешествия
    • Игры
    • Люди и Блоги
    • Юмор
    • Развлечения
    • Новости и Политика
    • Howto и Стиль
    • Diy своими руками
    • Образование
    • Наука и Технологии
    • Некоммерческие Организации
  • О сайте

Скачать или смотреть Historia ya Nguli wa mziki Mbaraka mwinshee aliyefia Mombasa Kisauni kwa kupata ajali ya barabarani.

  • Africa Daily Connect
  • 2022-07-08
  • 10562
Historia ya Nguli wa mziki Mbaraka mwinshee aliyefia Mombasa Kisauni kwa kupata ajali ya barabarani.
  • ok logo

Скачать Historia ya Nguli wa mziki Mbaraka mwinshee aliyefia Mombasa Kisauni kwa kupata ajali ya barabarani. бесплатно в качестве 4к (2к / 1080p)

У нас вы можете скачать бесплатно Historia ya Nguli wa mziki Mbaraka mwinshee aliyefia Mombasa Kisauni kwa kupata ajali ya barabarani. или посмотреть видео с ютуба в максимальном доступном качестве.

Для скачивания выберите вариант из формы ниже:

  • Информация по загрузке:

Cкачать музыку Historia ya Nguli wa mziki Mbaraka mwinshee aliyefia Mombasa Kisauni kwa kupata ajali ya barabarani. бесплатно в формате MP3:

Если иконки загрузки не отобразились, ПОЖАЛУЙСТА, НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если у вас возникли трудности с загрузкой, пожалуйста, свяжитесь с нами по контактам, указанным в нижней части страницы.
Спасибо за использование сервиса video2dn.com

Описание к видео Historia ya Nguli wa mziki Mbaraka mwinshee aliyefia Mombasa Kisauni kwa kupata ajali ya barabarani.

Wasifu wa nguli huyo unaeleza kuwa alizaliwa Juni 27, 1944 mjini Morogoro.
Mbaraka alikuwa na vipaji vingi vikiwemo vya kutunga na kuimba nyimbo ambazo zilikuwa zikiburudisha, zikielimisha na kutoa maonyo kwa jamii.


Mbaraka alikuwa bingwa wa kupiga gitaa la solo ambalo alilimudu hadi kufikia kuitwa ‘International Soloist’.Aidha aliweza kuongoza kwa ufanisi mkubwa bendi za Morogoro Jazz kwa bendi yake ya Super Volcano kwa miaka tofauti.


Mwinshehe alikuwa mtoto wa pili kuzaliwa kati ya watoto 12, kati yao ni yeye na wadogo zake Zanda na Matata ndio waliokuwa wanamuziki.Zanda alikuwa mwimbaji wa nyimbo za kizungu katika bendi ya Morogoro Jazz na Matata alikuwa akichanganya drums katika bendi hiyo hiyo.


Baba yake Mzee Mwinshehe Mwaruka alikuwa wa kabila la Waluguru, msomi aliyekuwa Karani katika mashamba ya Katani. Mama yake alikuwa wa kabila la Ngoni.


Kwa mujibu wa maelezo ya familia, babu yake Mbaraka alikuwa wa kabila la Wadoe kutoka Bagamoyo. Alipelekwa na Wakoloni kijiji cha Mzenga Kisarawe, mkoani Pwani akawe Chifu wa huko.


Baada ya kutawazwa kuwa Chifu, alioa wake tisa na kupata watoto zaidi ya 50 akiwemo baba yake Mbaraka, Mzee Mwaruka.


Tungo za nyimbo za Mbaraka zimejaa maudhui mema, ambazo zilimpandisha ‘chati’ hadi kuchaguliwa kuwa mmoja kati ya wasanii waliokwenda kuiwakilisha Tanzania katika mji wa Osaka nchini Japan mwaka 1970, ambako kulifanyika maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Expo70.


Tanzania iliwakilishwa na wasanii kadhaa akiwemo mzee Morris Nyunyusa, mlemavu wa macho, aliyekuwa na kipaji cha kupiga ngoma zaidi ya kumi kwa wakati mmoja.


Wengine walikuwa Wanasanaa toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kundi la Blass Band toka jeshi la Polisi lililokuwa likiongozwa na Mzee Mayagilo.


Aliporejea toka Japan, Mbaraka alitunga wimbo uitwao ‘Maonesho Japan’ akisimulia jinsi mafanikio makubwa yaliyopatikana katika maonesho hayo.


Kwa upande wa elimu Mbaraka Mwinshehe aliipata huko Kisarawe Middle School mwaka 1963.



Nguli huyu alikumbwa na mauti baada ya kupata ajali ya gari iliyoyafupisha maisha ya mwanamuziki huyo Januari 12, 1979.


Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo aliyejulikana kwa majina ya Zebedee Japhet Kinoka, maarufu kama Super Zex, alieleza kuwa kifo cha Mbaraka Mwinshehe kilitokea majira ya saa 7 mchana Januari 12, 1979 alipokuwa anatoka maeneo ya Kisauni, jirani na mji wa Mombasa.


Alisema kuwa mwanamuziki huyo alikuwa ameenda kumtembelea mtanzania mwenzake aliyekuwa akimiliki hoteli huko.


Kinoka alisema alipofika karibu na kanisa la Kongoya, aliliona gari aina ya Peugot 404, lenye rangi nyeupe likitoka upande wa Bush bar. Gari hilo lilikuwa katika mwendo mkali likaligonga roli moja lililokuwa likitokea upande mwingine. Watu walokuwa karibu wakakimbilia kungalia ajali akiwemo yeye.


Mara moja akamtambua Mbaraka na kuwambia watu kuwa huyo ni mwanamuziki Mtanzania anaitwa Mbaraka Mwinshehe.Iliwalazimu kuanza kukata mabati ili kumuondoa Mbaraka aliyekuwa amebanwa miguu katika gari lile akiwa bado yu hai.


Wakati kazi hiyo inaendelea Zebedee alikimbilia kwenye baa ya Kengeleni, ambako bendi ya Jamhuri Jazz ya Tanga ilkuwa ikitoa burudani ya muziki. Akawambia kuwa mwenzao kaumia sana, nao wakatoka mbio kwenda kushuhudia.


Walifanikiwa kumtoa Mbaraka kwenye gari hilo, akakimbizwa hadi katika hospitali ya Makadara, mjini Mombasa.Zebedee pia akatumwa kuwafuata wanamuziki wa bendi ya Super Volcano ambao wakati huo walikuwa wameanza kupiga muziki wa mwanzo wakimsubiri Mbaraka katika ukumbi wa baa ya Zambia.


Wanamuziki walipofika hospitalini hapo, wakaambiwa watoe damu ya kumuongezea kiongozi wao Mabaraka Mwinshehe.Kila mmoja akaanza kukwepa kutoa damu kwa visingizio mbalimbali. Baada ya muda mchache Mbaraka Mwinshehe akafariki dunia akiwa na umri mdogo wa miaka 34 tu!.


Mwili wa Mbaraka akasafirishwa hadi mpakani mwa Tanzania na Kenya ukapokewa na ndugu, jamaa, marafiki na maofisa wa Wizara ya Utamaduni.
Baadae mwili wa Mbaraka Mwinshehe akazikwa katika nyumba yake ya milele kijijini kwake Mzenga Wilayani Kisarawe, mkoa wa Pwani.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке

Похожие видео

  • MUHTAJ MUBARAK MWINSHEHE (Part Two) Kilichomsaidia baba alikuwa Msomi ndio maana alifanya vizuri.
    MUHTAJ MUBARAK MWINSHEHE (Part Two) Kilichomsaidia baba alikuwa Msomi ndio maana alifanya vizuri.
    3 года назад
  • Премьер-министр ликвидирован? / Немецкие военные атакованы
    Премьер-министр ликвидирован? / Немецкие военные атакованы
    16 часов назад
  • Mbaraka Mwinshehe  Morogoro Jazz Band EXPO 70
    Mbaraka Mwinshehe Morogoro Jazz Band EXPO 70
    8 лет назад
  • Mbaraka Mwinshehe & Super Volcano - Ukumbusho Volume 6
    Mbaraka Mwinshehe & Super Volcano - Ukumbusho Volume 6
    14 лет назад
  • МИХАИЛ УЛЬЯНОВ скрывал ЭТО от всех! Жуков, Высоцкий, дети - тайны ШОКИРУЮТ!
    МИХАИЛ УЛЬЯНОВ скрывал ЭТО от всех! Жуков, Высоцкий, дети - тайны ШОКИРУЮТ!
    18 часов назад
  • ⚡️Трамп РАЗНЕС Путина в ОБРАЩЕНИИ! Москва В УЖАСЕ: СРОЧНО СЛИВАЕТ Иран после ЗВОНКА
    ⚡️Трамп РАЗНЕС Путина в ОБРАЩЕНИИ! Москва В УЖАСЕ: СРОЧНО СЛИВАЕТ Иран после ЗВОНКА
    3 часа назад
  • DENIS MPAGAZE: Mfahamu SAMORA MACHEL Baba Wa Taifa La MSUMBIJI Na Harakati Za Ukombozi Wa Taifa Hilo
    DENIS MPAGAZE: Mfahamu SAMORA MACHEL Baba Wa Taifa La MSUMBIJI Na Harakati Za Ukombozi Wa Taifa Hilo
    3 года назад
  • Simba walinihonga lakini tukawafunga: Hamis Kinye, kipa wa zamani wa Yanga (WATANI WA JADI SPESHO)
    Simba walinihonga lakini tukawafunga: Hamis Kinye, kipa wa zamani wa Yanga (WATANI WA JADI SPESHO)
    7 лет назад
  • ПРАВДА О ЧИНГИСХАНЕ: ЭТО НЕ ИСТОРИЯ, ЭТО РАЗОБЛАЧЕНИЕ!!!
    ПРАВДА О ЧИНГИСХАНЕ: ЭТО НЕ ИСТОРИЯ, ЭТО РАЗОБЛАЧЕНИЕ!!!
    3 дня назад
  • MUHTAJ MUBARAK MWINSHEHE (Part One) Baba alipata Tuzo ya Golden Disc lakini hatukuwahi kuipata
    MUHTAJ MUBARAK MWINSHEHE (Part One) Baba alipata Tuzo ya Golden Disc lakini hatukuwahi kuipata
    3 года назад
  • SAMORA MACHEL: Rais Aliyetolewa UHAI Kwa Njama Kisa Mabeberu!
    SAMORA MACHEL: Rais Aliyetolewa UHAI Kwa Njama Kisa Mabeberu!
    6 лет назад
  • Kifo
    Kifo
    3 года назад
  • Что происходит внутри Ирана? | Варламов — о последствиях войны США и Израиля против Ирана
    Что происходит внутри Ирана? | Варламов — о последствиях войны США и Израиля против Ирана
    20 часов назад
  • Nani Anayesema Ukweli Juu Ya Kifo Cha Moringe Sokoine? Hii Hapa Historia Yake Mwanzo Mwisho (Part1)
    Nani Anayesema Ukweli Juu Ya Kifo Cha Moringe Sokoine? Hii Hapa Historia Yake Mwanzo Mwisho (Part1)
    3 года назад
  • TRUMP VITA IMEKWISHA, IRAN HAKUNA KUSIMAMISHA VITA
    TRUMP VITA IMEKWISHA, IRAN HAKUNA KUSIMAMISHA VITA
    23 часа назад
  • Mbaraka Mwinshehe - Shida
    Mbaraka Mwinshehe - Shida
    8 лет назад
  • Почему весь мир боится АЛИ ХАМЕНЕИ? Самый опасный лидер Ближнего Востока!
    Почему весь мир боится АЛИ ХАМЕНЕИ? Самый опасный лидер Ближнего Востока!
    19 часов назад
  • DR. REMI ONGALA: Uganga wa Kienyeji/ Muziki Damuni/ CONGO hadi TANZANIA
    DR. REMI ONGALA: Uganga wa Kienyeji/ Muziki Damuni/ CONGO hadi TANZANIA
    4 года назад
  • Nitamtuma Mshenga Mbaraka Mwinshehe  Morogoro Jazz Band
    Nitamtuma Mshenga Mbaraka Mwinshehe Morogoro Jazz Band
    8 лет назад
  • Mashemeji Wangapi by Mbaraka Mwinshehe
    Mashemeji Wangapi by Mbaraka Mwinshehe
    5 лет назад
  • О нас
  • Контакты
  • Отказ от ответственности - Disclaimer
  • Условия использования сайта - TOS
  • Политика конфиденциальности

video2dn Copyright © 2023 - 2025

Контакты для правообладателей video2contact@gmail.com