Maadhimisho ya Miaka 60 KKKT. Askofu Shoo asema Kanisa linaunga mkono Uwekezaji - Kuhusu Bandari.

Описание к видео Maadhimisho ya Miaka 60 KKKT. Askofu Shoo asema Kanisa linaunga mkono Uwekezaji - Kuhusu Bandari.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan amewashukuru kipekee, Mkuu wa Kanisa, KKKT Askofu Dr. Fredrick Onaeli Shoo na Askofu Dr. Benson Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe kwa mchango wao mkubwa katika kumshauri katika mpango wa kuleta Maridhiano (Reconciliation) hapa nchini.

Ametoa shukrani hizo katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kiinjili la Kilutheri Tanzania unaoendelea katika Chuo kikuu cha Tumain Makumira - Arusha ambao umeanza Agosti 21 mwaka huu.

Rais Samia ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, amesema kuwa katika mpango wake wa 4R (yaani R nne) ambazo ni Reconciliation, Reform, Resilience and Rebuild viongozi hawa wa kiroho wamemsaidia sana katika R ya kwanza Reconciliation ikimaanisha Maridhiano hapa nchini.

#kad
#karagwe
#kijitonyama
#ikulumawasiliano
#serikali
#bandari

Na: Merabu Birakashekwa.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке