RAIS SAMIA ACHARUKA 'UKIMYA WANGU SIYO UJINGA, KUROPOKA KWAO...TUMEVUMILIANA SANA

Описание к видео RAIS SAMIA ACHARUKA 'UKIMYA WANGU SIYO UJINGA, KUROPOKA KWAO...TUMEVUMILIANA SANA

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amejibu matamko ya balozi zinazowakilisha mataifa mbalimbali nchini, yaliyotaka uchunguzi wa haraka wa matukio ya utekaji na mauaji ya watu, akisema Tanzania ni nchi huru haipaswi kuelekezwa cha kufanya kwenye mambo yake. Katika majibu yake hayo, amewashutumu mabalozi hao akisema walichokitamka haamini kama ni maelekezo ya wakuu wa nchi zao, huku akiahidi kuwachongea kwa marais wa mataifa husika kwa kuiingilia Tanzania. Chimbuko la majibu ya mkuu huyo wa nchi ni tamko la pamoja la balozi za mataifa 15 yanayowakilisha Umoja wa Ulaya (EU) nchini, yakilaani na kutaka uchunguzi wa haraka na huru wa matukio ya mauaji.

Balozi zilizotoa tamko hilo la pamoja ni Ubelgiji, Uingereza, Canada, Denmark, Ufaransa, Finland, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Norway, Poland, Hispania, Sweeden na Uswisi.
Soma kwa undani kupitia tovuti ya Mwananchi

Комментарии

Информация по комментариям в разработке