Ukweli Kuhusu Mchele wa Plastiki Unavyotengenezwa Dar

Описание к видео Ukweli Kuhusu Mchele wa Plastiki Unavyotengenezwa Dar

Katika wiki za hivi karibuni, kumekuwa na uvumi una¬osambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, juu ya kuwepo kwa mchele wa plastiki, unaodaiwa kuingizwa nchini na wafanyabiashara wasio waaminifu, unaouzwa katika vibanda vya akina mama n’tilie.
Baada ya uvumi huo kuleta hofu kubwa kwa wananchi, hasa kufuatia video mitandaoni kuonyesha wali uli¬opikwa ukiliwa na hata kiwanda kina¬chodaiwa kuwepo nchini kinachoten¬geneza mchele huo, Risasi Jumamosi liliamua kuufanyia kazi uvumi huo ili kujua mbivu na mbichi ya sakata hilo.
Risasi Jumamosi liliambiwa kuwa mchele huo unauzwa katika baadhi ya masoko ya jijini Dar es Salaam yakita¬jwa kuwa ni pamoja na yale ya Bugu¬runi, Mwananyamala, Makumbusho na Afrikasana.
Kikosi kazi kilisambazwa katika masoko hayo na kufanya uchunguzi wake ikiwa ni pamoja na kuzungumza na baadhi ya wanaouza bidhaa hiyo.
Lucas Kimadi wa Soko la Makum¬busho anasema; “Hata hivyo, ingawa
nimesikia juu ya tetesi hizo kiuk¬weli sijawahi kuuona machoni mchele huo wa plastiki. Ila nime¬wahi kusikia siku za nyuma kuwa kuna wafanyabiashara walikuwa wanauingiza kinyemela na seri¬kali iliwachukulia hatua.”
Mfanyabiashara mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mwesigwa, alipoulizwa juu ya ku¬wepo kwa mchele huo, alisema anavyofahamu, hayo ni maneno ya mitandaoni, kwani hajawahi kuuona.
“ Sasa kama ni wa plastiki utaupikaje na uwe tayari kwa kula. Watu wameamua kuvumi¬sha tu lakini sidhani kama kuna ukweli katika hili, na ninakubal¬iana kabisa na TFDA pengine hiyo video ambayo tumeiona mtandaoni inaonesha namna ya kutengeneza mifuko.”
Hali kama hiyo ilikuwepo pia katika masoko yote ambako Global TV ilitembelea, kwani wafanyabiashara wote walionyesha kushangazwa kwao na madai hayo, wakisema hivi sasa baada ya mavuno, wanapata mchele mwingi kutoka Mikoa ya Mbeya, Rukwa, Morogoro na Mwanza na kwamba siyo rahisi kwao kuuza wala kununua mchele wa plastiki.
Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe    / uwazi1  
Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya…
   / uwazi1  
   / uwazi1  
   / uwazi1  
WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/
FACEBOOK:   / globalpublishers  
TWITTER:   / globalhabari  
INSTAGRAM:   / globalpublishers  

Комментарии

Информация по комментариям в разработке