MAPYA YAIBUKA UCHAGUZI WA TLS, NKUBA APINGA USHINDI WA MWABUKUSI ASEMA ANACHOTAKA KUFANYA

Описание к видео MAPYA YAIBUKA UCHAGUZI WA TLS, NKUBA APINGA USHINDI WA MWABUKUSI ASEMA ANACHOTAKA KUFANYA

Mgombea aliyeshika nafasi ya pili katika uchaguzi mkuu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Sweetbert Nkuba, amekataa kutambua ushindi alioupata mpinzani wake wa karibu, Wakili Boniface Mwabukusi kwa madai ya ukiukwaji wa mwenendo wa uchaguzi.
Nkuba ameyazungumza hayo leo Jumamosi Agosti 3, 2024 jijini Dodoma saa chache baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo.
Katika uchaguzi huo, Mwabukusi alipata kura 1,274 akifuatiwa na Nkuba aliyepata kura 807.

"Matokeo haya yaliyotangazwa siyatambui sababu kulikuwa na ukiukwaji wa mwenendo wa uchaguzi. Tayari nimejipanga na mawakili wangu kwa ajili ya kupinga matokeo haya mahakamani," amesema Nkuba

Комментарии

Информация по комментариям в разработке