TAJIRI AMFUNGIA MWANAFUNZI NDANI SIKU 3 ABAKWA KILA SIKU ASKARI ASHAWISHI RUSHWA LIISHE

Описание к видео TAJIRI AMFUNGIA MWANAFUNZI NDANI SIKU 3 ABAKWA KILA SIKU ASKARI ASHAWISHI RUSHWA LIISHE

Mwanafunzi wa Kidato cha kwanza shule ya Sekondary Somsom kata ya Kibosho magharibi wilaya ya MOSHI vijijini mwenye umri wa miaka (14) jina limehifadhiwa amebakwa na mtu afahamikaye kwa jina la Deogratias Felix Olomi marufu kama Sikinde (50) ambaye ni mfanyabiashara kijijini hapo.

Akisimulia tukio hilo mwanafunzi huyo amesema kuwa siku ya jumatatu tar 26 alikuwa anaenda shule asubuhi akakutana na Deo ambaye alimkamata na kumpeleka kwenye chumba chake na kumfungia hapo huku akiwa amefungulia radio sauti ya juu ili sauti ya mtoto isisikike wakati anapika kelele huku akimtishia kumuuwa endapo atapiga kelele.
Mwanafunzi huyo alifungiwa katika chumba hicho kuanzia jumatatu mpaka jumatano huku akilishwa mandazi na Soda bila mtu yeyote kufahamu akiwa anamuingilia kila siku bila mtu yeyote kujua lolote lakini siku hiyo ya jumatano akamfukuza alfajiri ili aende shule ndipo akapelekwa Nyumbani kwao.

Mama mzazi wa Mwanafunzi huyo Restusta Olomi akizungumza amesema kuwa baada ya kumpata mtoto wake walienda kituo cha polisi na kutoa taarifa kwamba wamempata mtoto ndipo askari wakamuambia atafute mgambo ili mtuhumiwa akakamatwe akafanya hivyo.
“Tulipomkamata tukamleta akafungiwa mahabusu afande akaniambia nimuachie shilingi elfu 20 ya kwa ajili ya kumpeleka mtuhumiwa kituo kikubwa nasisi tukaenda hospitali ya mawenzi tulipofika tukambiwa tukae nje na mtoto apimwe lakini Dokta akasema anayetakiwa kupewa majibu ni askari Tukampigia yule askari akaja alipofika akaniambia amemhoji mtuhumiwa na amekubali kwamba amebaka lakini amesema atatoa milioni ili jambo liishe nikakataa” Amesema mama wa Mtoto

Комментарии

Информация по комментариям в разработке