WATOTO WA DK NDUGULILE WAMZUNGUMZIA BABA YAO KWA HUZUNI, WAUTAJA WIMBO ALOKUWA ANAUPENDA

Описание к видео WATOTO WA DK NDUGULILE WAMZUNGUMZIA BABA YAO KWA HUZUNI, WAUTAJA WIMBO ALOKUWA ANAUPENDA

Watoto wa aliyekuwa mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Dk Faustine Ndugulile wamemzungumzia baba yao, huku wakikumbuka namna alivyokuwa karibu na familia hata katikati ya ratiba zake ngumu.
Ukaribu huo ulimfanya kutokuwa tayari kukosa sherehe yoyote ya familia, ikiwemo siku za kuzaliwa na mahafali.
Watoto hao wamesema hayo leo Jumatatu, Desemba 2, 2024 walipopata nafasi ya kuzungumza katika hafla ya kumuaga baba yao inayofanyika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Dk Ndugulile alifariki dunia usiku wa Novemba 27, 2024 nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu.
Alipoanza kuzungumza mtoto wake wa kike, Martha Ndugulile amesema amepoteza mwanga wake, nguzo yake, shujaa wake na kielelezo cha mtu aliyekuwa akimtazama katika vitu anavyofanya.
Kwa upande wake, mtoto Melvin alisema baba yake alikuwa jasiri, mpenda watu, mkarimu, mwenye akili huku kwake atabaki kuwa baba bora zaidi.
“Namshukuru Mungu kwa kunipa baba na nitakuwa naye moyoni hata katika kutokuwepo kwake, ingawa hayupo nasi kimwili, nitampenda zaid. Kwa hakika, nikianza kutaja kila kitu alichonifanyia na familia yetu katika miaka yangu 18 ya maisha, sidhani kama nitaweza kumaliza.
“Najua kwa hakika baba yangu alikuwa kilele cha mafanikio mengi nchini Tanzania, Afrika na duniani. Aliweka rekodi ambazo hazijavunjwa. Alijijengea urithi wake mwenyewe,” amesema

Комментарии

Информация по комментариям в разработке