Zorah - Tunapendezana (Official Lyric Video)

Описание к видео Zorah - Tunapendezana (Official Lyric Video)

Kuna wakati changamoto za maisha na utafutaji zinaweza kupelekea mahusiano kuyumba na muda mwingine kuvunjika kabisa💔🥀

Lakini ukiwa na mtu, mnayesikilizana, kuombeana na kuamini kuwa kesho yenu ni bora kuliko leo, huyo ni mtu sahihi sana kwako, mnapendezana!💐🌹🫶

#TUNAPENDEZANA sasa inapatikana katika Digital Platforms zote Duniani🌍

Sikiliza hapa: https://linktr.ee/Zorah_

Follow Zorah on Social Media: 

Subscribe on Youtube:    / @zorah_  

Instagram: https://instagram.com/raj_zorah?igshi...

Facebook: https://www.facebook.com/profile.php?...

TikTok: tiktok.com/@rajzorah

Twitter: https://x.com/raj_zorah?t=uSkaSR0eVRT...

TUNAPENDEZANA LYRICS

(Kassu)

Najua ushanivumilia mambo kibao
Lakini haukuchoka ukakang'ang'ana na mie
Na sio kiangazi masika na sie tutafika (nivumilie)
Na maisha matuta kama nikianguka (ninyanyue)

Ila simaanishi nimefeli, kwangu mambo bado
Walishanikwamisha matapeli, wakaharibu mambo
Na usije wakakurubuni kwa punje za mtama, ukaniacha mie

Nitakulinda nitakutunza ka' mboni ya jicho langu
Na sitojali mangapi wanasema wanateta
Maana..

Tunapendezana
ooh iwe kwa shida na raha
Tutaongozana
mi na wewe hata tukilala njaa
Tunapendezana
mmh wawili kama mapacha
Tutaongozana
ooh mi na wewe baby

#INSTRUMENTAL 

Najua sometimes unawaza hulali
Mawazo maswali nitapata lini (nitapata lini)
Kumekuchosha uswahilini nyumba za kupanga
Ndani joto kali (ndani joto kali)

Na kuna muda naota wamekubeba wenye mali unaishi Masaki
Hakuna ndoto iliyoboa ile siku nakufuma napigwa risasi
Na hakuna siku nitaumia sana kama itakupoteza nafsi (itakupoteza nafsi)

Na usije wakakurubuni kwa punje za mtama, ukaniacha mie
Nitakulinda nitakutunza ka' mboni ya jicho langu
Na sitojali mangapi wanasema wanateta

Maana..

Tunapendezana
tunapendezana mi na wewe
Tutaongozana
wawili tu tutaongozana milele
Tunapendezana
tunapendezana mi na wewe kama mapacha
Tutaongozana
tutaongozana (aaaahh aaaaahh) 
Tutaongozana 
mi na wewe.. kama mapacha

#INSTRUMENTAL 

(Kassu)


#zorah #kassumusic #bongofleva #bongoflava
#bongo #music #tunapendezana

© Kassu Music • All Rights Reserved

Комментарии

Информация по комментариям в разработке