KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 03/03/2026
MAFUNGO YA KWARESMA 2026 - SIKU YA 12
NENO KUU:
Mhubiri 3:1
Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.
Matendo 3:19
Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;
MADA:
"KUTOKA MISIMU MPAKA KUSUDI" (FROM SEASONS TO REASON)
UJUMBE WA LEO :
UPAKO WA MAANDALIZI KATIKA MISIMU
SHABAHA:
1. Kujua kwamba kuna upako maalumu wa kimaandalizi katika kila msimu wa maisha, na upako huo unalenga kukusaidia na kukuandaa ili uvuke salama na kufikia kusudi.
2. Kupokea upako unaoachiliwa katika msimu uliopo na faida zake.
1 Samweli 16 : 1, 13
1 Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.
13 Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.
Zaburi 78 : 70 - 71
70 Akamchagua Daudi, mtumishi wake, Akamwondoa katika mazizi ya kondoo.
71 Nyuma ya kondoo wanyonyeshao alimwondoa, Awachunge Yakobo watu wake, na Israeli urithi wake.
Matendo 13 : 36
36 Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.
1. UPAKO WA MAANDALIZI JUU YA DAUDI NA MISIMU ALIYOPITIA.
Zaburi 89 : 20 - 23
20 Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu.
21 Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu.
22 Adui hatamwonea, Wala mwana wa uovu hatamtesa.
23 Bali nitawaponda watesi wake mbele yake, Nitawapiga wanaomchukia.
Matendo 1 : 8
8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
KAZI ZA UPAKO WA KATIKA MISIMU
2. KUKUINULIA WATU WA MSAADA.
1 Samweli 18 : 1 - 5
1 Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe.
2 Sauli akamtwaa siku ile, wala hakumwacha arudi tena nyumbani kwa baba yake.
3 Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe.
4 Ndipo Yonathani akalivua joho alilokuwa amelivaa, akampa Daudi, na mavazi yake, hata na upanga wake pia, na upinde wake, na mshipi wake.
5 Basi Daudi akatoka kwenda kila mahali alikotumwa na Sauli, akatenda kwa akili; Sauli akamweka juu ya watu wa vita; jambo hili likawa jema machoni pa watu wote, na machoni pa watumishi wa Sauli pia.
1 Nyakati 12 : 1, 21 - 22
1 Basi hawa ndio wale waliomjia Daudi huko Siklagi, alipokuwa akijificha kwa ajili ya Sauli, mwana wa Kishi; nao walikuwamo miongoni mwa wale mashujaa, waliomsaidia vitani.
21 Wakamsaidia Daudi juu ya kile kikosi kilichomshambulia; kwani walikuwa waume mashujaa wote, nao wakawa maakida jeshini.
22 Maana siku kwa siku humjia Daudi watu wa kumsaidia, hata wakapata kuwa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.
Wagalatia 2 : 9
9 tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;
AGENDA ZA MAOMBI
1. Omba Mungu akupe upako wa kukuandaa na kukuvusha msimu uliopo ili ufikie kusudi.
2. Omba Mungu akupe upako utakaokutambulisha kwa wengine ili upate msaada kwenye msimu uliopo.
Mhubiri : Mwl. Benjamin Abel.
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com
Информация по комментариям в разработке