Kibonge Wa Yesu - Neno Moja (Official Music Video) SMS Skiza 8021080 to 811

Описание к видео Kibonge Wa Yesu - Neno Moja (Official Music Video) SMS Skiza 8021080 to 811

Mawazo ya mwanadamu wakati Mwingine ni ya kukata tamaa lakini Mungu anaweza kusimama na kauli yake Moja tu inayoweza kubadili hatima ya Mwanadamu na kurejesha vilivyopotea na kuhuwisha vilivyokufa. Wimbo huu ukawe wa Urejesho na uponyaji wa majeraha kwa kila moyo uliyoumizwa na kukosa tumaini Mungu akawe Msaada kwako katika Jina la Yesu. Amen!🙏
John 5:5-6
Audio produced by ​⁠‪@kstarrecords255‬
Video directed by @mrazalia
Bvg : Nuru mwaipungu

Get it on ALL DIGITAL PLATFORMS
Listen to NENO MOJA by Kibonge Wa Yesu
On Boomplay: https://www.boomplaymusic.com/share/m...
On Audiomack: https://audiomack.com/kibonge-wa-yesu...

©2024KiboMelodies.All rights Reserved.

#kibongewayesu #gospelmusic #NenoMoja #Semanenomoja

Verse 1

Kauli yako moja tu inaweza kubadili hatima
kauli yako inabadilisha mambo
kauli yako moja inaweza kunitengeneza
vilivyo kufa kwangu vikachipuka tena
na nimekuja hapa Mungu na uchumi wangu ulioyumba, afya yangu nafsi yangu uvihuwishe tena

kuna muda nakubali huenda sababu ni mimi mwenyewe
ule muda najikwaa kwa kufuata yangu na kukuacha wewe
uliempa ndege uwezo wa kupaa angani haya matatizo,shida kwako ni kitu gani?
uliempa samaki uwezo apumue majini haya masimango,mateso ebaba tupilia mbali

Hook:

Nikakuomba Mungu nakuomba kama kulia nimelia sana inatosha
ninakuomba Mungu nakuomba kama kuchekwa nimechekwa sana inatosha
baba Mungu wangu wee
.
Chorus:

Sema neno Moja
ninakuomba useme
nipo tayari kupokea
kwa neno lako ntapona Yesu
sema neno moja
kwa neno lako ntashinda mie
nipo tayari kupokea
baba Mungu wangu wee
sema neno moja
ninakuomba useme
nipo tayari kupokea
kwa neno lako ntapona Yesu
sema neno moja
kwa neno lako ntashinda mie
nipo tayari kupokea

Verse 2

kama batimayo nipo kando ya njia
Ooh Baba
nakusubiri useme ili nione
Ooh Baba
japo nimesikia mengi ya kunikatisha tamaa ila neno lako moja linaweza niinua tena
Nimeomba sana mpaka wanasema ninapiga kelele
ila sichoki bado nakazana kukusubiria wewe
kama kukwama nimekwama
na kiza kimetanda
nategemea neno lako nuru liniangazie
kama msaada sijaona kwa watu wadunia
nategemea ulie juu unisadie

hook :

Nikakuomba Mungu nakuomba kama kulia nimelia sana inatosha
ninakuomba Mungu nakuomba kama kuchekwa nimechekwa sana inatosha
baba Mungu wangu wee

Chorus:

sema neno moja
ninaomba useme
nipo tayari kupokea
kwa neno lako ntashinda
sema neno moja
mhh
nipo tayari kupokea
kwa neno lako nitainuka tena
sema neno moja
neno la baraka
nipo tayari kupokea
neno neno lako
sema neno moja
neno la kunitajirisha
nipo tayari kupokea
litanipa amani
neno litanifariji

Комментарии

Информация по комментариям в разработке