BREAKING: MCHEKESHAJI MKONGWE MZEE PEMBE AFARIKI DUNIA

Описание к видео BREAKING: MCHEKESHAJI MKONGWE MZEE PEMBE AFARIKI DUNIA

Mwigizaji na Mchekeshaji Mkongwe Nchini Tanzania, Mzee Yusuph Kaimu maarufu Pembe amefariki dunia jioni ya leo October 20,2024 katika Hospitali ya Temeke Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Baadhi ya Waigizaji akiwemo Vicent Kigosi (Ray) na Mau Fundi wametoa taarifa za msiba huo na kusema taratibu za mazishi zitatolewa baadaye, @AyoTV_ imeongea pia na Katibu wa Chama cha Waigizaji Kinondoni, Jafari Makatu ambaye amethibitisha na kusema “Alikuwa anaumwa alilazwa Temeke Hospital, amefariki kama saa moja iliyopita, alilazwa kama siku tatu nne, na tulikuwa tumepanga kwenda kumuona Kesho baada ya kuambiwa anaumwa”

#AyoTV na millardayo tunatoa pole kwa Waigizaji, Wachekeshaji, Ndugu, Jamaa na Marafiki na wengine wote walioguswa na msiba huu, Mungu amlaze pema Ndugu yetu Pembe. 🙏🏿💔

Комментарии

Информация по комментариям в разработке