JE UNAFAHAMU KUHUSU UNYWAJI WA POMBE KUPITA HAJA KUBWA? ..ISIKUPITE HII NI HATARI "ALCOHOL ENEMA"

Описание к видео JE UNAFAHAMU KUHUSU UNYWAJI WA POMBE KUPITA HAJA KUBWA? ..ISIKUPITE HII NI HATARI "ALCOHOL ENEMA"

#kenya #ntv #pombe #alcohol #enem #hatari
Alcohol enema: Vijana wanywa pombe kupitia haja kubwa
ALCOHOL ENEMA/ KUNYWA POMBE KWA NJIA YA HAJA KUBWA..

Maisha yapo kasi sana. Kila mmoja hutumia pombe kwa sababu mbalimbali- siko hapa kueleza sababu ya kila mmoja maana sifahamu, kila mmoja anayo yake.

Wakati wengine wakitumia pombe kupitia mdomo kama kiburudisho na starehe yao. Wapo waliokuja na njia mbadala ya kutumia pombe.

Wao walikaa na kutaka kupingana na vile mwili unafanya kazi na kwakugundua jinsi mmeng'enyo wa chakula ufanyavyo kazi basi wakaamua kuukimbia kinamna.

Wao hunywa pombe kupitia njia ya haja kubwa. Usishangae, wala hujasoma vibaya. Namaanisha wanatumia njia ya haja kubwa kunywa pombe.

Hapa hutumia bomba za sindano ama mfano wa pamba laini iliyolowanishwa katika pombe, wapo wanaotumia Tampon-wanatumia baadhi wanawake wakiwa hedhi kama pedi . Wengine huenda mbali na kutumia chujio maalumu kwaajili ya kuweka pombe katika njia ya haja kubwa.

Kwa kufanya hivyo ni wazi huwa wanaepuka pombe isifike katika ini na kuvunjwa vunjwa na kufanya kupoteza makali yake.

Vijana wengi kwa sasa imekuwa ndiyo mtindo wao. Vijana wengine wakike wamekuwa wakitumia mpaka uke kufanya kitendo hicho.

Nitakupa kidogo elimu ya juu juu.

Mtu anapokunywa pombe kwa mdomo huwa inaenda tumboni na baadae hufyonzwa kuingia katika mzunguko wa damu na kufika katika ini. Huko kuna kimeng'enyaambacho kinafanya pombe huvunjwa hunjwa na kupunguzwa makali yake. Lakini huyu anayetumia njia ya haja kubwa huwa pombe haipiti kwenye ini.

Kunywa pombe kwa njia ya haja kubwa kuna ruka njia ya kwanza ya kimetaboliki- FIRST PASS METABOLISM(sintogusa huku mambo ya dehydrogenase) na kufanya pombe iingie kwenye mzukungo kama ilivyo.

Njia ya haja kubwa huwa imejaaliwa kuwa na mishipa mingi ya damu, vile vile maji hufyonzwa katika utumbo mpana hivyo kufanya pombe kufyonzwa kwa haraka na kuingia katika mzunguko wa damu kupitia kufyonzwa katika kuta za utumbo mpana.

Watu hutumia njia hii kwa mambo yao. Mfano wapo wanaotumia kwa kutaka kulewa haraka, wapo wanaoepuka harufu kali ya pombe vinywani mwao. Kwasababu watatumia njia ya haja kubwa basi hawatatoa harufu ya pombe mdomoni, Wapo wanaodai kukwepa kining'inia(Hangover) Sababu nyingine nyingi wanazijua wao wanaotumia njia hii.

Kitendo hiki kinaweza hatarisha afya kama mtu atatumia pombe kwa kiwango kikubwa. Madhara atakayoyapata ni kama; kuchanganyikiwa, kutapika, joto kushuka, kuishiwa maji n.k

Njia hii inaweza sababisha mambo kama; kutokwa damu njia ya haja kubwa kutokana na michubuko ya pombe, vidonda na maambukizi katika njia ya haja kubwa.

Baadhi ya vijana imekuwa ni njia yao mpya katika kujipatia burudani. Pamoja na yote bado tahadhali inaendelea kutolewa juu ya njia hii ya hatar
Hakuna jipya chini ya jua. Kitendo hiki hakijaanza jana wala ju. Kimeanza tangu enzi hizo huko kwa watu wa Maya.

Makala haya ni kwaajili ya kujifunza na wala si kuchochea mtu kufanya kitendo hiki.

Haya ni machache katika mengi niliyokumegea. Unaweza tenga muda ukafuatilia zaidi.

#zuchu #bongo #trending #trandkenya #trandingshorts

Комментарии

Информация по комментариям в разработке