WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI KIGOGO WA MABASI YA MWENDOKASI, AWAITA MAKATIBU WAKUU OFISINI KWAKE

Описание к видео WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI KIGOGO WA MABASI YA MWENDOKASI, AWAITA MAKATIBU WAKUU OFISINI KWAKE

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Suzana Steven Chaula baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Akizungumzia kuhusu Mtendaji Mkuu wa wakala huo, Mhandisi Ronald Rwakatare, Waziri Mkuu amesema suala hilo atalikabidhi kwa Mamlaka ya uteuzi.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo leo (Jumatatu, Aprili 19, 2021) wakati alipotembelea kituo cha Kikuu cha DART-Gerezani ambapo alionesha kutoridhishwa na utendaji wa viongozi hao.

“Tangu Mtendaji Mkuu ameingia DART ana miaka mitano hakuna hata basi moja alilonunua, na anasema hana fedha kwani abiria hawasafiri si kila siku wanapigania kule Kimara na wote wanalipa unasemaje hakuna fedha ya kununulia magari”.

Waziri Mkuu amesema kuwa tangu mradi huo ulipoanza mabasi yamekuwa yakipungua kutoka 140 hadi 85. “Watendaji wapo tu wamekaa ofisini wanapigwa na AC (viyoyozi) wananchi wanaumia. Hatuna sababu ya kumbakiza mtu kama hafanyi kazi”.

Amesema wakala huo ulianzishwa na Serikali kwa ajili ya kuondoa adha ya usafiri kwa wananchi lakini viongozi hao wameshindwa kusimamia vizuri na hivyo kusababisha mradi huo kutoendelea vizuri.

Waziri Mkuu amesema mapato mengi ya Serikali yamekuwa yakipotea kutokana na uendeshaji wa wakala huo. “Kwa nini ukatishaji wa tiketi haufanyiki kwa njia ya kielektroniki kwa asilimia 100? Tiketi zinauzwa kwa vifurushi.”

Комментарии

Информация по комментариям в разработке