MWANZO MWISHO TUKIO LA AJALI YA HELKOPTA ILIYO MUUA RAIS WA IRAN || MABAKI YALIONEKANA

Описание к видео MWANZO MWISHO TUKIO LA AJALI YA HELKOPTA ILIYO MUUA RAIS WA IRAN || MABAKI YALIONEKANA

Televisheni ya taifa ya Iran imethibitisha kifo cha Rais wa nchi hiyo Ebrahim Raisi aliyefariki dunia kwenye ajali ya helkopta iliyotokea hapo jana Mei 19, 2024.

Taarifa inasema pia Raisi alikuwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Hossein Amir-Abdollahian ambaye pia amefariki dunia wakati walipokuwa wakirejea kutoka nchi jirani ya Azerbaijan kwenye hafla ya uzinduzi wa bwawa.

Wawili hao wamefariki baada ya ajali hiyo iliyotokea eneo la milimani katika jimbo la East Azerbaijan, ijapokuwa chanzo hakijatajwa lakini inaelezwa hali mbaya ya hewa ya ukungu ilikuwa imeenea eneo hilo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la IRNA, wengine waliokuwemo ndani ya helikopta hiyo ni pamoja na Gavana wa Mkoa wa Azerbaijan Mashariki, Malek Rahmati wa Iran na mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Mkoa wa Azerbaijan Mashariki, Ayatollah Mohammad Ali Ale-Hashem pamoja na walinzi.

Hata hivyo, vikosi vya uokoaji ambavyo vilipata shida kufikia eneo la ajali kutokana na ukungu na mvua, lakini baadaye vilipata mabaki ya helikopta hiyo kando ya mlima.

Mkuu wa Shirika la Hilali Nyekundu la Iran, Pir Hossein Kolivand, amesema waokoaji walipoona mabaki hayo, walisema hakuna dalili za uhai.

Serikali bado haijatoa tamko rasmi lakini shirika la habari la IRNA limesema kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kimeitishwa kikiongozwa Makamu wa Rais Mohammad Mokhber baada ya tukio hilo.

Kwa mujibu wa Katiba ya Iran, iwapo Rais atafariki akiwa madarakani, kifungu cha 131 kinasema makamu wa kwanza wa Rais ndiye atakayeshika madaraka huku baraza linalojumuisha makamu wa kwanza wa rais, spika wa bunge na mkuu wa mahakama lazima lipange uchaguzi wa Rais mpya ndani ya muda usiozidi siku 50.

Kiongozi mkuu wa nchi hiyo, Ayatollah Ali Khamenei amewataka Wairani wasiwe na wasiwasi kuhusu uongozi akisema nchi itaendelea bila usumbufu.

Salamu za rambirambi zimeanza kutolewa akiwemo, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi aliyesema kwenye X kwamba, ‘ameshtushwa na kifo hicho cha kutisha’ huku akitaja mchango wake katika kuimarisha uhusiano wa pande mbili za India na Iran utakumbukwa daima.


Imeandikwa na Sute Kamwelwe kwa msaada wa mashirika ya habari ya kimataifa.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке