Watalii wa Ukraine wakwama Zanzibar

Описание к видео Watalii wa Ukraine wakwama Zanzibar

Serikali ya Zanzibar imesema inashirikiana kwa karibu na ubalozi wa Ukraine uliopo nchini Kenya kuangalia ni namna gani itawasafirisha watalii wa Ukraine wapatao elfu moja ambao hivi sasa wamekwama kisiwani humo baada ya kuzuka kwa vita kati ya Urusi na Ukraine.

Waziri wa Utalii wa Zanzibar Leila Mohammed Musa amemwambia mwandishi wa BBC Aboubakar Famau kwamba, watalii hao, tayari wanaendelea kupewa huduma za kibinadamu licha ya wengine kuwa wamemaliza siku zao za kutalii.

#bbcswahili #tanzania #zanzibar #Ukraine

Комментарии

Информация по комментариям в разработке