ZOP YA KAMILISHA KAMPENI KWA MAFANIKIO

Описание к видео ZOP YA KAMILISHA KAMPENI KWA MAFANIKIO

ZOP yakamilisha kampeni ya kijana kwa kijana kwa mafanikio
taasisi ya Zanzibar outreach program kupitia vijana waliomaliza kidatu cha sita waliokuwa wakipita katika skuli mbalimbali za mkoa wa mjini magharibi kuelimisha jamii kuhusu saratani ya matiti imekamilisha kampeni hiyo skuli ya sekondari jang'ombe kwa mafanikio makubwa.
Akizungumza mwalimu wa skuli hiyo maalim bi Asha amesema imewasaidia kujitambua na kujichunguza hatua za awali za saratani ya matiti .
Kwa upande wao wakufunzi wa mafunzo hayo wamesema wamekamilisha kampeni yao bila kupitia vikwazo na kuwashukuru walimu wa skuli walizo pita kwa mapokezi mazuri ya ujumbe walioutoa.
Nao wanafunzi wa skuli ya jang'ombe wameahidi kuifanyia kazi elimu waliyopewa kwani imewafumbua macho juu ya janga la saratani ambalo linauwa mamia ya watu ulimwenguni.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке