ZIARA YA MHE. MTANDA KATA YA CHILANGALA

Описание к видео ZIARA YA MHE. MTANDA KATA YA CHILANGALA

Ziara ya Mbunge wa jimbo la Newala Vijijini Mhe. Maimuna Mtanda imeendelea tena leo July 24, 2024 katika kata ya Chilangala ambapo amefanya mikutano ya hadhara katika vijiji vyote tano vya kata hiyo kuwaeleza utekelezaji wa ilani ya CCM 2020/25, kupokea kero zao ili kuzitafutia ufumbuzi na kuwakumbusha kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.

Wananchi wa kata hiyo wameonekana kumpokea Mhe. Mtanda kwa bashasha kutokana na utekelezaji mkubwa wa ilini ulivyo fanyika katika kata yao kwani kwasasa wanapata huduma ya maji, afya ,umeme, barabara na miradi ya shule huku wakimpongeza na kumshukuru kutokana na kazi nzuri anayoifanya katika kutatua kero zao ambapo wanachama wawili wa CUF kutoka Kijiji cha Mnyengachi na Miyuyu wamerudisha kadi za chama chao na kujiunga na CCM.

Katika ziara hiyo Mhe Mtanda ametoa kiti mwendo kwa Anifa Nurudini Ismaili ambae ana ulemavu ili kimsaidie kwenye kutembea huku akiendelea kutimiza ahadi yake kwa vikundi vya ngoma na kwaya ambao waliomba fedha kwaajili ya kununua sare za vikundi vyao na kuendelea kutoa mipira kwa timu za vijana wakike na wakiume zilizopo kwenye vijiji hivyo.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке