#ikulu #raissamia #uvccmtaifa #ikuluzanzibar #uvccmmwanza #rcmwanza #rsmwanza #wazirimkuu #bungedodoma #tanzaniahabari #thtv #wizarayamamboyandani #wizarayaujenzi #bungelatanzania #tamisemi #ofisiyamakamuwarais #ofisiyawazirimkuu #tls #mahakama #takukuru
KESI YA UHUJUMU UCHUMI YA ABDI WARSAME HIRSI WANAOSHTAKIWA KWA MAKOSA 841 YAPIGWA KALENDA
Kesi namba 2330 ya mwaka 2026 inayowakabili Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Salaaman Health Serives Ltd, Abdi Warsame Hirsi na Meneja Rasilimali Watu, Elia Adam Makongwa wanaoshtakiwa kwa makosa 841 ya utakatishaji fedha na uhujumu uchumi, imehairishwa hadi Machi 18, mwaka huu itakapotajwa tena.
Shauri hilo limehairishwa leo Machi 4, 2026 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Erick Maley baada ya kutajwa kwa mara ya nne.
Upande wa mashtaka katika shauri hilo umewakilishwa na mawakili wa serikali, Fadhili Mwandoloma na Jaines Kihwelo huku washtakiwa wakiwakilishwa na wakili, Allan Robi.
Ambapo, shauri hilo limeletwa leo kwa ajili ya ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kufanya mazungumzo ya makubaliano na washtakiwa (Plea Bargaining) juu ya mashtaka yanayowakabili, lakini mazungumzo hayo yameshindikana baada ya DPP kuomba yasogezwe mbele.
Akitoa hoja ya kuomba kuhairisha mazungumzo hayo mahakamani hapo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Fadhili Mwandoloma amesema upande wa jamhuri umepokea maelekezo kutoka ofisi ya DPP kuhairisha mazungumzo hayo mpaka yatakapotoka maelekezo mengine.
“Ni kwa sababu upande wa mshtakiwa umewasilisha malalamiko ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi na ofisi ya DPP, na mwanasheria wa mshtakiwa wa kwanza yuko Dodoma anashughulikia jambo hilo,” amesema Mwandoloma.
Baada ya hoja hiyo, wakili wa washtakiwa hao, Allan Robi amekubaliana na hoja na kuiomba mahakama ihairishe shauri hilo kwa siku chache ili kupata mrejesho wa mazungumzo yanayoendelea na ofisi ya DPP.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Erick Maley baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili amehairisha shauri hilo hadi Machi 18, 2026 litakapotajwa tena na kupata mrejesho wa hatua iliyofikia ili mazungumzo kwa ajili ya Plea Bargaining yaendelee.
“Tunashukuru kwa ajili ya timu ambayo ilikuwa tayari kwa hiki kikao (plea bargaining) na imefika mahakamani, lakini ni kwa sababu hili liko nje ya uwezo wetu, msife moyo muwe tayari itakapopangwa tarehe nyingine tuone kam hayo yatakuwa yamefikia hatua nzuri tuendelee na mazungumzo haya,” amesema Hakimu Maley.
Hata hivyo, baadhi ya maofisa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mahakama walikuwepo mahakamani hapo kwa ajili ya mazungumzo ya Plea Bargaining.
Washtakiwa hao, miliki wa Kampuni ya Salaaman Health Services Ltd, Dk. Abdi Hirsi Warsame na Afisa Rasilimali watu, Elia Adam Makongwa wanashtakiwa kwa makosa 841 ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.
Wakituhumiwa kuusababishia hasara Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni moja kati ya mwaka 2021 na 2023 kupitia genge la uhalifu lililofanya kazi mkoani Mwanza na Dar es Salaam.
Информация по комментариям в разработке