Huyu ndiye Clatous Chama

Описание к видео Huyu ndiye Clatous Chama

USAJILI wake ulifanyika dakika za mwisho
ikiwa ni saa kadhaa kabla ya Simba kupaa
zake Uturuki kuweka kambi ulidhaniwa kuwa
ni wa kawaida.
Kama kawaida Mwanaspoti ndio lililofichua
ujio wake. Hata siku wachezaji wa Simba
walipopimwa afya kwenye Taasisi ya Jakaya
Kikwete pale Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
alifanyiwa vipimo na majibu yake
yalionyesha yupo kamili gado kukimbizana na
kina Kelvin Yondani, Andrew Vincent
(Yanga), Aggrey Morris (Azam FC) na Yusuf
Ndikumana wa KMC.
Lakini kabla ya hapo mashabiki wa Simba
walikuwa hawaifahamu shughuli yake kwani,
mabosi wao walifanya dili lake kimyakimya.
Huyu anaitwa Cletus Chama.
Jamaa ni fundi wa mpira kwani, anafahamu
jinsi ya kuuchezea na kubwa zaidi ni uwezo
wake wa kupiga pasi za mwisho. Katika
mechi ya kirafiki kati ya Simba na Asante
Kotoko ya Ghana kwenye Tamasha la Simba
Day, ndipo mashabiki wa Simba wakaelewa ni
kwa nini mabosi wao walifanya usajili wa
Chama bila ya makelele mengi.
Chama alicheza dakika zote 90 za mchezo huo
ikabainika ni kwa nini mashabiki wa Simba
hawana mzuka tena na kiungo wao fundi
waliyemnasa kutoka Yanga, Haruna
Niyonzima. Mzambia huyo amemuondoa
kabisa Niyonzima kwenye mioyo ya
mashabiki na viongozi wa Simba kwani,
shughuli yake uwanjani sio ya kitoto
unaambiwa.

Fundi wa Pasi

Katika mechi moja tu ambayo Chama
amecheza huku akiwa amesajiliwa kwa
mkataba wa mwaka mmoja ameonesha ni
fundi wa kupiga pasi kama zinavyotakiwa
kwa mastraika wake.
Dhidi ya Asante Kotoko
Alikuwa ikipiga pasi za chini ambazo zilifika
mahala husika na hata muda mwingine
alikuwa ikipiga pasi ndefu kwa mawinga wa
kushoto na kulia.
Umahiri wa kukaba wa viungo wakabaji wa
Simba, James Kotei na Jonas Mkude ulimfanya
Chama kuonekana fundi zaidi katika eneo hilo
kwani, kwenye mchezo huo mashabiki
walikuwa wakipagawa kila Chama alipokuwa
na mpira.
Chama ni mzuri katika zile pasi za kampa
kampa tena ambazo zinaweza kupigwa katika
viwanja vichache tu hapa Tanzania kwani,
vingi havina maeneo mazuri ya kuchezea na
huenda akishindwa kuonekana bora katika
hilo.
Pasi za mwisho
Upele ulipata mkunaji katika mechi ya Asante
Kotoko, Chama alipiga pasi za mwisho
takribani tano ambazo washambuliaji wa
Simba walichotakiwa kufanya ni kupasia tu
nyavuni kisha kukimbia kwenye kona
kushangilia na mashabiki.
Chama amemuonyesha Kocha Patrick
Aussems kuwa ana vitu adimu kwenye miguu
yake na ambavyo vikitumika vizuri, basi
ukikutana na Simba utapigwa bao za kutosha
tu kama ataendelea kuwa kwenye kiwango
kama cha juzi Jumatano.
Uwezo wa kuachia mipira na kuupitisha
kwenye eneo lolote analotaka ili kumfikia
mshambuliaji anayemtaka. Hilo litakuwa
likiwaumiza sana mabeki wa timu pinzani.
Pasi za Chama ni sahihi na zina macho.
Fundi wa kukokota
Ni wazi kabisa kiungo yeyote bora wa
ushambuliaji lazima awe na uwezo wa
kumiliki mpira ili kuanzisha mashambulizi
kwa timu pinzani. Kwa hili Chama utamtaka
ubaya kwani analifanya tena kwa ufasaha
zaidi. Chama ana uwezo wa kumiliki mpira
akianziwa kutoka kwa viungo wakabaji au
mabeki na mara chache kupoteza mipira
hiyo.
Wakati akipokea mipira, ana uwezo wa
kukokota kwa hatua 20 kutoka nyuma na
kwenda mbele au kubadili kutoa upande
mmoja na kupeleka mwingine.
Kwa chenga pia mbaya
Chama mbali ya uwezo aliokuwa nao wa
kumiliki, kukokota na kupiga pasi ana kitu
kingine cha ziada kwa kuwa na uwezo wa
kupiga chenga.
Katika mechi dhidi ya Kotoko, Chama
aliwapiga chenga mabeki na kupiga pasi za
maana, jambo ambalo liliwafanya mashabiki
wa Simba jukwaani kupiga kelele tu kila
wakati wakishangilia.
Hata hivyo, Kocha Aussems atakuwa na kazi
ya kuhakikisha hampi majukumu mengi ya
kupiga chenga kwani hilo linaweza kuwa na
madhara kwa Chama akikutana na Yondani
anaweza kuingia kwenye orodha ya majeruhi.
Kama Pogba tu
Kiungo wa Kifaransa wa Manchester United,
Paul Pogba ni bonge la mchezaji lakini,
amekuwa akitifuana na kocha wake, Jose
Mourinho kila wakati.
Moja ya mzozo wao hutokana na kukataa
kubebeshwa majukumu ambayo sio yake
uwanjani, kukaba.
Mourinho anamtaka Pogba akabe, achezesha
timu na kusukuma mashambulizi mbele
jambo ambalo anatakiwa kulifanya kwa
wakati mmoja uwanjani.
Hilo, linaweza kuwa tatizo kubwa kwa
Chama, ambaye uwezo wake wa kukaba bado
unaonekana ni tatizo.
Chama sio mzuri wa kukaba pindi timu
inapopoteza mpira na katika mchezo huo, hilo
lilionekana wazi kabisa.
Sio fundi wa kupoteza mipira, lakini
inapotokea mpira uko chini ya timu pinzani,
basi Chama huonekana akikimbiakimbia tu
badala ya kusaidia kukaba kama anavyokuwa
kwenye kushambulia.
Kwa kile kilichotokea dhidi ya Kotoko,
huenda Kocha Aussems akafanya mabadiliko
ili kumwezesha Chama kucheza eneo huru
kwa ajili ya kuanzisha mashambulizi.
Msimu mpya haujaanza lakini Chama
ameonyesha atakuwa mchezaji muhimu
kwenye kikosi cha Kocha Aussmea na huenda
angekuwa mchezaji wa kawaida ama kukaa
benchi kama angekuja wakati wa Mfaransa
Pierre Lechantre, ambaye ni muumini wa
soka la kujilinda zaidi.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке