Karibu katika Ibada ya Jumapili, Siku ya Bwana ya Pili kabla ya Majilio
▶ SOMO: JIANDAE KWA HUKUMU YA MWISHO
MATHAYO 25: 14 - 30
..................
ZABURI 16: 8 - 11
8. Nimemweka BWANA mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuliani mwangu, sitaondoshwa.
9. Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nayo nafsi yangu inashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
10. Maana hutaitupa kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.
11. Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako kuna furaha tele;
Na katika mkono wako wa kulia
Mna mema ya milele.
2 WATHESALONIKE 1: 3 - 10
3. Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi.
4. Hata na sisi wenyewe tunaona fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya subira yenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na dhiki mnazostahimili.
5. Ndiyo ishara hasa ya hukumu iliyo haki ya Mungu, ili mhesabiwe kuwa mwastahili kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa.
6. Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi;
7. na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake,
8. katika muali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu;
9. watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;
10. yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu).
MATHAYO 25: 14 - 30
14. Maana itakuwa kama mfano wa mtu aliyetaka kusafiri, akawaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.
15. Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.
16. Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.
17. Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida.
18. Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake.
19. Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.
20. Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida.
21. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
22. Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida.
23. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
24. Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nilitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;
25. basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako. 26Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
27. basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
28. Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.
29. Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.
30. Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Hukumu kwa mataifa
▶ MHUBIRI: REV. CHARLES MZINGA
.........
👇👇
// NAMBA ZA SADAKA //
▶ LIPA KWA [ M-PESA] - 579 579 4
▶ NAMBA YA MPESA - 0757 - 391 - 174
JINA: KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
▶ MAENDELEO BANK
A/C NO 0137 9274 6021
JINA: LUTHERAN CHURCH AZANIA FRONT CATHEDRAL
TUFUATILIE KWENYE MITANDAO KWA TAHARIFA ZAIDI:
Instagram page: / kkkt_azaniafrcathedral
Website: https://www.azaniafront.org/
Facebook: / kkkt-azania-front-cathedral-101434162039079
#azaniafrontcathedral #ibada #lunchhour #morningglory #sundayservice #lutheran
Информация по комментариям в разработке