Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) inaendelea kusukuma mbele jitihada za mapinduzi ya kilimo nchini kwa kutekeleza miradi mikubwa ya umwagiliaji inayolenga kuboresha maisha ya wakulima, kuongeza uzalishaji na kuimarisha usalama wa chakula.
Katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Shinyanga pekee, zaidi ya wakulima 4,650 wananufaika moja kwa moja kupitia miradi hii, huku ekari 9,750 zikitarajiwa kumwagiliwa. Hatua hii inaleta matumaini mapya kwa jamii zinazotegemea kilimo kama uti wa mgongo wa maisha yao.
Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Raymond Mndolwa, amesema Serikali inaendelea kusimamia zaidi ya miradi 780 ya umwagiliaji nchini yenye thamani ya takribani trilioni 1.2. Hadi sasa miradi 126 ipo chini ya wakandarasi, zaidi ya shilingi bilioni 492 zimetumika, miradi 30 imekamilika kwa zaidi ya asilimia 80 na mingine 60 imepiga hatua ya zaidi ya asilimia 50 ya utekelezaji.
Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa mabwawa ya Membe, Mahiga na Nyida ambayo yanatarajiwa kubadilisha maisha ya maelfu ya wakulima. Katika mkoa wa Dodoma, bwawa la Membe litahifadhi maji kwa ekari 6,175 na kuhudumia wakulima 1,500, sambamba na skimu ya umwagiliaji yenye ekari 988 kwa wakulima 650. Pia nyumba 75 za wakulima vijana walionufaika na mradi wa Building a Better Tomorrow (BBT) zimeanza kujengwa.
Kwa upande wa Mwanza, mradi wa Bwawa la Mahiga utaondoa changamoto ya mafuriko katika Kijiji cha Mahiga wilayani Kwimba na kuwahudumia zaidi ya wakulima 1,000 katika ekari 1,235, wakilima mara mbili kwa mwaka hatua itakayoongeza kipato na usalama wa chakula. Mkoani Shinyanga, ujenzi wa bwawa la Nyida umekuwa suluhisho la ukame uliodumu kwa muda mrefu, ambapo wakulima 1,500 watanufaika na ekari 1,235, na sasa wataweza kulima mara tatu kwa mwaka kwa mazao ya mboga na matunda.
Mbali na mabwawa, Serikali imeanzisha mpango wa kitaifa wa kuchimba visima 67,500 katika halmashauri 184 ndani ya miaka nane. Mpango huu unatarajiwa kuwanufaisha zaidi ya wakulima 100,000, kila mmoja akimwagilia wastani wa ekari 2.5. Kwa mwaka huu wa fedha, visima 1,300 vinachimbwa katika mikoa 16 kwa kutumia mitambo mipya ya kisasa iliyopatikana na tayari imeanza kazi.
Baadhi ya wanufaika wameeleza kuwa miradi hii ya mabwawa na visima imeleta suluhisho la uhakika, si tu kwa kilimo bali pia kwa kupunguza mafuriko na kuongeza kipato cha kaya. Aidha Serikali inalenga kumwagilia ekari milioni 12.5 ifikapo mwaka 2030, kutoka milioni 3 za sasa. Dhamira hii inaakisi ajenda ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuleta maendeleo jumuishi, shamba kwa shamba na familia kwa familia.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Tufuatilie kupitia mitadao yetu ya kijamii
Instagram: https://www.instagram.com/nirc_tz?igs...
Facebook: / tumeyaumwagi. .
XTwitter: https://x.com/nirc_tz?t=UoFluCQyTUnM4...
LinkeInn: / tume-ya-taifa-ya-umwagiliaji-national-irri...
_______________________________________________________________________
#01trending #tanzania #umwagiliaji #kilimo #kilimobiashara #kilimochaumwagiliaji #MAKALA #story #storybook #ikulumawasiliano #DktSamiaSuluhuHassan #Rais #agriculture #agranews #agranewstoday #agricultural #agronomia #agroecologie #agriculturelife #agriculturalmachinery #kilimoufugaji #agrieconomy #kilimo #trendingtanzania #ikuluzanzibar #ikulutanzania #ikulu #ccm #ccmtz #chamachamapinduzi #agrfilms #agrf2023 #cnbctv #cnbcnews #kbcchannel1 @TBC_Online @ikulutanzania5474 @globaltv_online @kilimotv1730 @millardayoTZA @uhondotv5210 @WatchTanzania @Channeltenonline @CLOUDSMEDIA @chamachamapinduzi-official2767 @CNBC @CNN @bbcswahili7924
Информация по комментариям в разработке