VIONGOZI WA DINI TUMIENI MAJUKWAA YENU KUHAMASISHA LISHE BORA

Описание к видео VIONGOZI WA DINI TUMIENI MAJUKWAA YENU KUHAMASISHA LISHE BORA

VIONGOZI WA DINI TUMIENI MAJUKWAA YENU KUHAMASISHA LISHE BORA

Na WAF – Dodoma.

Serikali kupitia Wizara ya Afya imewataka viongozi wa dini nchini kuendelea kutumia fursa ya majukwaa ya dini kuielimisha na kuiamasisha jamii juu ya masuala ya lishe na mtindo bora wa maisha ili kufikia adhma ya kuboresha Afya na ustawi wa Watanzania.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Lishe Bi. Neema Joshua kutoka Wizara ya Afya akimwakilisha Mkurugenzi wa Kinga, Julai 18, 2024 jijini Dodoma wakati akifungua Kikao cha Kuhakiki na Kupitisha Maudhui ya Jumbe yaliyopo kwenye Rasimu ya Mwongozo wa Viongozi wa dini wa kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu masuala ya lishe nchini.

Bi. Neema amesema Wizara ya Afya inatambua nafasi na ushawishi mkubwa wa viongozi wa dini katika jamii, hivyo Wizara itaendelea kushirikia na viongozi wa dini kufanikisha adhima hiyo kwa kuandaa mwongozo utakaotumika kutoa elimu na hamasa ya masuala ya Lishe kupitia majukwaa ya dini katika jamii.

“Tunategemea michango yenu yenye tija itakayosaidia kuhakikisha mwongozo huu unakuwa na maudhui yanayokidhi mahitaji ya jamii yetu, ushirikiano wenu katika hatua hii ni muhimu sana na tunaomba muendelee kutuunga mkono kwenye safari hii ya kuboresha afya na ustawi wa jamii zetu kupitia kuelimisha na kuhamasisha masuala ya lishe kwa Watanzania”. Ameeleza Bi. Neema.

Aidha, ameeleza kuwa Tanzania inakabiliwa na changamoto ya utapiamlo ikiwemo lishe pungufu, upungufu wa vitamini,madini na lishe ya kuzidi hivyo serikali inaendelea kuweka mikakati ya kupambana na lishe duni kwa jamii.

“Takwimu za mwaka 2022 zinaonesha kuwa asilimia 30 (watoto 3 kati ya 10) walio na umri chini ya miaka mitano wamedumaa, asilimia 12 (mtoto 1 kati ya 10) walio na umri chini ya miaka mitano wana uzito pungufu hali inayoweza kusababisha magonjwa ya mara kwa mara, athari mbaya za ukuaji na ustawi wao kwa ujumla. Watoto wenye utapiamlo hawakui ipasavyo kimwili, kiakili na kisaikolojia na huwa na uwezo mdogo wa kufaulu masomo yao shuleni”. Ameeleza

Kwa upande wake Askofu Joseph Mpalagu amesema ili kuongoza waumini katika ibada ni lazima kuongoza waumini wenye Afya bora na kuahidi kuutumia muongozo huo katika kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu lishe bora ili kufikia lengo la Pamoja la kuwa na jamii yenye Afya bora.

"Kwenye maandiko ya Mungu biblia inasema miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu hivyo miili yetu ni sehemu ya kufanyia ibada hivyo inahitajika kuwa ni miili yenye afya nzuri, akili yenye ubunifu mzuri kwa ajili ya huduma za kiroho, hivyo baada ya kupitishwa kwa muongozo huu tunaahidi kwenda kuwafundisha waumini wetu”

MWISHO.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке