SIMBA SC 3-1 NKANA FC; FULL HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (CAF CL - 23/12/2018)

Описание к видео SIMBA SC 3-1 NKANA FC; FULL HIGHLIGHTS & INTERVIEWS (CAF CL - 23/12/2018)

Simba SC imefuzu kuingia hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya leo kuichapa Nkana FC magoli 3-1 katika mchezo wa maruadiano uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Matokeo hayo yameifanya Simba ifuzu hatua hiyo kwa jumla ya mabao 4-3 kufuatia kufungwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Zambia wiki moja iliyopita.

Katika mchezo wa leo Nkana ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 17 kupitia kwa Walter Bwalya akimalizia kwa mpira ambao mabeki wa Simba waliuzembea kwa kufanya mchezo wa kuotea.

Simba walitulia na kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Jonas Mkude dakika ya 29, kabla ya Meddie Kagere kupachika bao la pili kwa kichwa dakika ya 45 na baadaye dakika ya 88, Clatous Chama kuipa Simba bao la ushindi.

Baada ya kuaga mashindano haya, sasa Nkana FC wanakwenda kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo watalazimika kupitia hatua ya mchujo ili kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa barani Afrika.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке