DOTTO MAGARI ATAFUTA MDHAMINI, ARUDI SHULE / HATA KAMA UNAISHI GOROFANI HESHIMU WATU

Описание к видео DOTTO MAGARI ATAFUTA MDHAMINI, ARUDI SHULE / HATA KAMA UNAISHI GOROFANI HESHIMU WATU

"Nafanyiwa vitu vingi vya ajabu sana kwenye hii dunia, wapo watu wananichokoza!. Wananikasirisha!. Wananitukana kwenye mitandao. Nikipost Wana- comments vitu vya ajabu. Ili mradi tu wanakutoa kwenye mood lakini kwa sababu maisha ya mtaani ndio nilioanza nayo nayafurahia. Na yale maneno yao mabaya ndio yananisogeza mbele. Wananiambia simuwezi mtu fulani napandisha kioo cha gari naendelea na maisha yangu!"- @dotto_magari


"Wanawake hawanipendi kwa sababu nina mdomo. Mimi sipendwi na Slsina mambo ya mashangazi kwa sababu nina mdomo. Shangazi ukija kwangu ujipange. Pia upendeze, unukie"- @dotto_magari


"Uwe unaishi Mbinguni, au ghorofani. Uko nyuma ya mtu gani. Au kuna mtu ana kusikiliza au Mzee wako alikuwa nani! Heshimu watu!! Hata ukimkuta muokota makopo mpe Elfu Moja kama huna muache na maisha yake. Sio unamuona unaanza kusema anaiba side mirror ya gari, maisha hayapo hivyo! Usimuhukumu mtu kwa sababu maisha yake yapo tofauti na wewe"- @dotto_magari

"Hata sasa natamani kurudi darasani nisome. Nawaongelea wasomi kwa sababu naipenda elimu. Ninavyoongea vile naumia kwa sababu sijajijua. Ningeijua elimu wala nisingeizungumzia. Najitahidi sana niijue elimu. Na wasomi nawapeda kwa sababu wananisomeshea wanangu. Si mnamuona anaongea Kiingereza? Na wasomi ndio waliotuajiri. Na ndio wanatuambia tuamke Saa 12, sasa kwanini niwachukue? Nawapenda sana"

"Akitokea mtu akijitolea kunisomesha narudi darasani ni nijue lugha ya Kiingereza. Ambayo watu wananisema kila wakati. Sijui Kiingereza. Na ukishajua hii lugha vitu vingine utavijua. Kuna watu hawajasoma lakini lugha inawafanya waonekane wamesoma"- @dotto_magari

Комментарии

Информация по комментариям в разработке