Kipindi cha Ujuzi ni Maisha Mafunzo ya Utengenezaji wa Bidhaa za Ngozi

Описание к видео Kipindi cha Ujuzi ni Maisha Mafunzo ya Utengenezaji wa Bidhaa za Ngozi

Tanzania inafahamika miongoni mwa nchi zinazoongoza kuwa na mifugo mingi barani Afrika na hivyo kuwepo kwa uzalishaji mkubwa wa ngozi ambayo hutumika kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile viatu, mikoba na mikanda.

Mahitaji ya bidhaa zinazotokana na ngozi ni makubwa nchini ambapo bidhaa hizo hutumiwa na karibu kila mwananchi.

Pamoja na mahitaji yaliyopo, bado kuna changamoto ya uzalishaji wa bidhaa za ngozi zenye ubora ndani ya nchi. Miongoni mwa mambo yanayosababisha changamoto hiyo ni ukosefu wa wataalamu wa kuzalisha bidhaa hizo kwa kiwango bora.

Katika jitihada za kutatua changamoto hiyo, VETA kupitia chuo chake cha Dakawa ilianzisha utoaji mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi ili kuandaa wataalam watakaoweza kuleta mapinduzi katika sekta ya ngozi.

Katika kipindi hiki tutaangazia kwa undani juu ya mafunzo hayo na namna yanavyoandaa nguvu kazi itakayoweza kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kukidhi mahitaji ya soko hilo nchini n ahata nje ya nchi.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке