Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua waliohusika kifo cha Baraka

Описание к видео Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua waliohusika kifo cha Baraka

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Kagera, Yusuph Daniel amesisitiza kuwa jeshi halitasita kuwachukulia hatua waliohusika na kifo cha Baraka Lucas (20) ambaye mwili wake uliopolewa ziwani katika Kisiwa cha Goziba ukiwa unaelea majini.

“Tunaendelea na uchuguzi kubaini chanzo cha mauaji ya Baraka, haijalishi hata kama ni mtumishi wetu au ni mwananchi, taratibu za kisheria zitazingatiwa ili achukuliwa hatua. Wananchi naomba wawe watulivu maana wanahisi kifo cha kijana huyo ameuawa,” amesema Kamanda Daniel.

Mwili wa Baraka ulikutwa ziwani Jumatano Juni 12, 2024 katika Kisiwa cha Goziba ukielea wakati siku tatu kabla ya kifo chake alikuwa akishikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo cha Goziba baada ya kukamatwa kwenye doria saa saba usiku Juni 10, 2024.

Paschal Ibrahim, mkazi wa Goziba na baba mdogo wa Baraka, amesema wao kama familia ya marehemu wanaitaji kujua kwa nini aliyepelekwa mahabusu anaonekana tena ziwani akiwa amekufa.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке