PUMZI YA UHAI - LIVE MINISTRATION - RGCM SINGERS

Описание к видео PUMZI YA UHAI - LIVE MINISTRATION - RGCM SINGERS

Kila unapopata nafasi ya kumtumikia Mungu katika eneo lolote ichukulie kwa umuhimu na upekee maana umepata upendeleo kwa Mungu miongoni wa watu wengi na kwa sababu hiyo fanya kwa uhodari na bidii nyingi.

Ukishindwa kufanya hivyo, Mungu atawainua akina Daudi watakaofanya vema zaidi yako (Sauli) na isivyo bahati wenda ukashindwa kupata nafasi tena mbele za Mungu.

Wimbo huu ukupe nafasi ya kujitathimini upya juu ya utumishi wako mbele za Mungu , kubwa zaidi uhusiano wako na Mungu. Kwani mahusiano yako na Mungu ni ya muhimu kuliko utumishi wako mbele za watu.

Utumishi mbele za Mungu si tu kushika kipaza sauti na kuhubiri ila kazi zote zinazojenga ufalme wa Mungu hapa duniani ikiwa ni pamoja na kuhubiri injili ya kweli, kusimama na kazi ya Mungu kwa ujuzi, maarifa na elimu yako kama Bezaleli, pia kwa kutoa muda na mali zako kama vile fedha.

Kuwatumikia wengine katika nafasi za huduma, uongozi, utaalamu wa masuala mbalimbali kama afya na mambo mengine mengi. Tunakuombea uwe na utayari wa kumtumikia Mungu pasina kujali gharama maana Mungu atakuwa na wewe hata kukushangaza.

Please,

Like - Comment - Share - Subscribe.

Karibu.

Комментарии

Информация по комментариям в разработке