Maajabu: Show ya Kwanza ya R.O.M.A Mkatoliki Tangu Alipotekwa

Описание к видео Maajabu: Show ya Kwanza ya R.O.M.A Mkatoliki Tangu Alipotekwa

Roma Mkatoliki, usiku wa Eid el Fitr alikinukisha kinomanoma kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhiem kulipokuwa na shoo kubwa ya Nishushe Dar Live ambapo aliweka rekodi ya aina yake.
Shoo hiyo iliyopambwa na wakali kibao, wakiwemo Mr Blue, Snura na Darassa ambaye alimfungulia pazia Roma aliyekinukisha kinomanoma jukwaani hapo na kuzikonga vilivyo nyoyo za mamia ya mashabiki waliokuwa wamefurika ukumbini hapo.
Yaani mpango mzima ulikuwa ni bandika bandua, Mr Blue wakati akishuka jukwaani mkali wa kibao cha Maisha na muziki (Darassa) alivamia jukwaa na kibao chake hicho kisichokubali kuchuja ambapo hakuonekana mtu aliyethubutu kukaa wakati mkali huyo akikamua.
Darassa aliposhuka jukwaani umati wa mashabiki ulianza kusikia sauti ya Roma ikiimba kibao cha Viva Roma Viva huku mwenyewe wakiwa hawamuoni.
Mashabiki hao wakisubiria kumuona mkali huyo upande anaotokea walipigwa na butwaa baada ya kumuona akitokea angani na vazi jeupe kama malaika akishushwa na winchi iliyokuwa na chombo maalum kama kibanda ambacho mkali huyo alikuwa ndani yake.
Tukio hilo lilionekana kuvuta hisia za mashabiki hao walisikika wakisema kuwa halijawahi kutokea bongo.
Aliposhushwa alikamua vibao vyake mbalimbali ikiwemo vilivyowahi kutamba enzi hizo.
Akiendelea kukamua ghafla Stamina alimuibukia jukwaani kwa usafiri wa Bajaj ambapo wote wakajumuika kugonga shoo pamoja.
Mashabiki wakimshangaa Stamina kuvamia jukwaa kwa staili hiyo ghafla Rais wa Manzese kutoka kundi la Tip Top Connection, Madee naye alipanda jukwaani kama sapraiz kuungana na Roma na Stamina ambapo mambo yalikuwa mpaka majogooo.

Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe    / uwazi1  
Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya…
   / uwazi1  
   / uwazi1  
   / uwazi1  
WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/
FACEBOOK:   / globalpublishers  
TWITTER:   / globalhabari  
INSTAGRAM:   / globalpublishers  

Комментарии

Информация по комментариям в разработке